Wakazi wa kitongoji cha Kasangakanyika kilichopo kijiji cha Lupa maketi katika kata ya Ifumbo wanakwenda kuondokana na changamoto ya mawasiliano kupitia ujenzi wa mnara wa mawasiliano unaojengwa katika Mlima Igalawa uliopo katika kitongoji hicho hali itakayo rahisisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano muda wote.
Hayo yamezungumzwa na Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe. Masache Njelu Kasaka wakati akizungumza na kusikiliza kero za wananchi katika kitongoji cha Kasangakanyika kilichopo kijiji cha Lupamaketi Kata ya Ifumbo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Maisha ya sasa hivi ni maisha ya mawasiliano ya simu za mkononi usipokuwa na mawasiliano unakuwa umepoteza fursa mbalimbali ambazo ungeweza kuzipata .Tunaendelea kuboresha hilo na ninavoongea na ninyi hapa tunakwenda kuwajenga mnara hapa katika Mlima Igalawa na vifaa tayali vimeshaletwa vipo kwenye ofisi ya Mtendaji wa kata ili kuwa na uhakika wa mawasiliano hapa masaa ishirini nan ne(24)”alisema Mhe. Masache.
Aidha Mhe.Masache amewapongeza wanachi na wadau wa kitongoji cha KasangaKanyika kwakwendelea kujitoa kwa hali na mali katika ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kunza ujenzi wa Shule ambapo ameahidi kuwaunga mkono kwa kuwachangia mifuko hamsini (50) ya saruji ili iweze kuwasaidia ujenzi huo .
Atupakisye Mwansembo mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa niaba ya Wananchi wengine amempongeza Mhe. Masache kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wake wa Kitongoji cha Kasangakanyika na kata ya Ifumbo kwa ujumla na kuomba utekelezaji kwa mambo mbalimbali ambayo Wananchi wameyaomba .
“Sisi tunakupongeza pamoja na kamati zako kutoka Wilaya na kata kwasababu maendeleo tunayaona ,tunakuomba twendelee kushirikiana pamoja na wewe ili vitu hivi vikamilike kwasababu tukianza kwa moto tukarudi kuwa baridi tutakuwa hatujafanya chochote , usijiulize kwanini niko hapa mama wa CHADEMA ni kwasababu Malaria bila Mseto haijapona bado sisi tuko pamoja na wewe tunachotaka ni viongozi bora na sio bora viongozi”alisema Atupakisye.
Ziara ya Mhe. Mbunge ya kuzungumza na kutatua kero mbalimbali za wananchi imefanyika katika ngazi za Vitongoji ikijumuisha viongozi wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya , kata, kijiji na kitongoji pamoja Wanachi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Mhe.Masache Njelu Kasaka akizungumza na wananchi wa katika kitongoji cha Kasangakanyika kijiji cha Lupamaketi kata ya Ifumbo wakati wa ziara yake ya kuzungumza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ngazi za vitongoji.
Atupokisye Mwasembo Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akimpongeza Mhe. Mbunge kwa niaba ya Wananchi kutokana na juuhudi kubwa anazozifanya za kuwaletea Wananchi wake Maendeleo.
Baadhi ya Wananchi wa kitongoji cha Kasangakanyika wakimsikiliza Mhe. Masache Njelu Kasaka juu ya utekelezaji wa miradi malimali ya maendeleo uliofanyika na unaoendelea kufanyika katika kitongoji hicho na kata ya Ifumbo kwa ujumla.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.