Kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya PREMIUM itagharimia masomo ya Shule ya Upili (A’ Level) wanafunzi wawili watakaofanya vizuri masomo yao kwa kupata daraja la kwanza katika mtihani wao wa kidato cha nne mwaka 2024.
Akizungumza wakati wa Ziara iliyoratibiwa na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Kipembawe ndugu Kassim Kirondomara, Mkuu wa kitengo cha TEHEMA kutoka kampuni ya Premium Tanzania Bi Delister Hyera amesema Kampuni yake imeamua kuwekeza kwa vijana kwaajili ya Taifa la sasa na la kesho
“Si mmeniahidi mtafaulu vizuri? Sasa na mimi natoa zawadi kwa kaka mmoja na dada mmoja atakayepata daraja la kwanza (Division one) tutalipia ada kwa kidato cha tano na kidato cha sita lakini na mimi nitakuwa na zawadi yangu binafsi kwa mdada atakayefanya vizuri, nitamshonea sare za Shule (uniform) kokote anatakokwenda kusoma masomo yake ya ‘A level’ niwaombe mtunze ahadi hizo” Amesema Bi Hyera
Awali akiwasilisha mada yake Afisa tarafa wa Tarafa ya Kipembawe ndugu Kassim Kirondomara amesema namna pekee ya kubadiri ugumu wa Maisha wanaokabiliana nao wazazi wa wanafunzi walioko Shuleni hasa wale wa Kidato cha nne 2024 ni kusoma kwa bidii ili wafaulu mtihani waon hatimaye waendelee na masomo ya Juuu.
“Matokeo yenu ya mwaka jana yalikuwa sio ya kuridhisha kabisaa kwani zaidi ya asilimi 80 ya wanafunzi walimefeli, na matokeo yenu ya mtihani uliofanyika mwezi mei hayaakisi malengo ya wilaya yetu na mkoa wetu na hata upande wenu hayawapeleki kokote ambapo wanafunzi zaidi ya mia moja wamepata daraja la nne na daraja sifuli huku wanafunzi watatu tu wakiwa wamepata daraja la tatu, hakuna daraja la pili na hakuna daraja la kwanza, Nimeumia sana.” Alisema Kirondomara
Aidha Kirondomara alimekumbusha wanafunzi juu ya Shughuli kuu ya uzalishaji mali inayofanywa na wazazi wa wanafunzi wengi Tarafa ya Kipembawe kwamba ni kilimo cha Tumbaku kwa kusisitiza ugumu wa kazi hiyo amewataka wanafunzi kuongeza bidii sana katika maandalizi ya mitihani yao ili baadaye waweze kuzikomboa familia zao.
“Nimeambiwa hapa kwamba mmemaliza mada zote katika masomo yote, na nimeambiwa mmefanya mtihani wa Kanda matokeo yake yataletwa hivi karibuni, nitafurahi kuona matokeo yanabadirika ukilinganisha na yale ya awali na tuanze kuondoa ziro kwani wewe unayepata ziro maana yake unafanana na mtu ambaye hajasoma kabisa. Niwakumbushe Wazazi wenu wanafanya kazi Ngumu sana ili kuhakikisha wewe unasoma na unafikia malengo yako na wewe ndiye unatarajiwa kubadirisha maisha magumu ya familia yako nyumbani na namna sahihi ya kufanikisha hilo ni kufaulu mitihani yako ili uende hatua nyingine za kielimu” aliendelea kuongeza Kirondomara
Baada ya mawasilisho mbalimbali kutamatika wanafunzi wakiongozwa na Afisa Tarafa wa tarafa ya Kipembawe wamekula kiapo ya kuhakikisha wanapata daraja la kwanza, daraja la pili na daraja la tatu, huku kipo hicho kikieleza hakuna mwanafunzi atakayepata daraja la nne na daraja sifuri
“Sisi wanafunzi wa Kidato cha Nnne (wakitaja Shule zao) tunaahidi ya kwamba hatupata daraja Sifuli wala daraja la nne, mtu atakaye feli atapata daraja la tatu, wengine tuliobaki tutapata daraja la pili na daraja la kwanza. Tunaahidi kwako afisa tarafa na viongozi meza kuu wote. Na tuaahidi kwa wazazi wetu walioko Nyumbani kwamba tunapata daraja la kwanza mpaka daraja la tatu ili tuweze kuenda kidato cha tano. EEE Mwenyeezi MUNGU tusaidie”
Afisa tarafa wa tarafa ya Kipembawe Ndugu Kassim Kirondomara yuko kwenye ziara ya kuhamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii ili kufika hatma njema ya Maisha yao ili hapo baadaye waweze kukomboa familia zao kutoka katika hali duni. Katika Ziara hiyo amekuwa akiongozana na wadau mbalimbali wakiwepo Kampuni za ununuzi wa Tumbaku, viongozi wa Serikali na wadau wengine
Bi. Delister Hyera Mkuu wa kitengo cha TEHEMA kutoka Kampuni ya ununuziwa Tumbaku ya Premium akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtanila wakati wa Ziara ya Kuhimiza wanafunzi kusoma kwa bidii
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Nne Shule ya Sekondari Mtanila wakifuatilia kwa makini Maelekezo na mafunzo wakati wa Ziara iliyoratibiwa na Afisa tarafa wa tarafa ya Kipembawe
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.