Mkuu wa wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mhe. Mbaraka Alhaji Batenga ameagiza kamati zote za ujenzi zinazosimamamia Miradi mbalimbali ya Ujenzi wilayani Chunya zijengewe uwezo wa kusimamia miradi husika ili watakapokiuka maelekezo waweze kuchukuliwa hatua kwa haki kwa mujibu wa Kanuni, Taratibu na Miongozo
Ametoa agizo hilo jana tarehe 29/1/2024 wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa Zahanati ya Igundu ambapo Zaidi ya milioni hamsini (50,000,000) zimepelekwa kujenga miundombinu mbalimbali ikiwepo tanki la maji, vinawia mikono, vyoo na kichomea taka
“Wajumbe wote wa kamati za ujenzi wajengewe uwezo wa kusimamia miradi hiyo kabla ya kukabidhiwa jukumu la kuanza kusimamia mradi husika jambo ambalo litasaidia wajumbe hao kusimamia ipasavyo mradi husika na hata kuhakikisha ukamilifu wa mradi huo” alisema Mhe.Batenga
Aidha Mhe Batenga ameuagiza uongozi wa Afya kuzingatia ushauri uliotolewa na Wakala wa maji na Usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) pamoja na TANESCO ili kuhakikisha wananchi wa Igundu wanaendelee kutatua changamoto zote maana hilo ndio lengo la Serikali kusogeza miradi mbalimbali kwa wananchi wake wakiwepo wananchi wa wilaya ya Chunya
Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Kaimu Mganga Mkuu Edward Tengulaga alisema siku saba zinatosha kuhakikisha kibao kinachoonesha huduma zinazotolewa katika zahanati hiyo kinawekwa pamoja na kibao kinachoonesha uwepo wa Zahanati eneo hilo vitu ambavyo vilibainishwa kwamba ni muhimu na havikuwepo ili kuwarahishsia wananchi ambao sio wenyeji watakapohitaji huduma hiyo
Ziara ya Mkuu wa wilaya ililenga kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika kata ya Sangambi ambapo alitembelea pia mradi wa Maji Igundu, mradi wa ujenzi wa vyoo katika Shule ya msingi Sangambi, mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya pamoja na kukagua hali ya mazingira katika kitongoji cha Tukuyu
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mrakibu mwandamizi wa Uhamiaji Mhe Mbaraka Alhaji Batenga akizungumza baada ya kukagua mradi wa maji Igundu wakati akiwa ziara ya kukagua miradi kata ya Igundu
Mkuu wa wilaya ya Chunya akipokea taarifa ya ujenzi wa mradi wa kituo cha Afya Sangambi alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika kata ya Sangambi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.