Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya imetambua mchango wa kamati za ujenzi katiika miradi ya Maendeleo inayojengwa katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya huku akiwashukuru kwa juhudi kubwa wanayofanya katika usimamizi wa Miradi hiyo
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule Mpya ya awali na Msingi inayojengwa kwenye eneo la Shule ya Sekondari Sangambi Jana 14.1.2026 Mwenyekiti amesema wanastahili pongezi sana
“Naomba niwapongeze sana Viongozi wa Sangambi hasa wale wote waliojitambulisha kama wanakamati wa Kamati za Ujenzi, tunawapongeza sana kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yenu, Niwaombe muendelee kuwa na moyo huu hata wakati wa utekelezaji wa miradi mingine”Alisema Mhe. Nshinshi
Aidha Mhe. Nshinshi amewaomba Jeshi la Polisi hasa kituo cha Polisi Sangambi kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi wa kata ya Sangambi katika nyanja mbalimbali ikiwepo Matumizi ya Vyomba vya moto, kwani wananchi hao wanategemea sana vyombo hivyo katika shughuli zao za kila siku za kujitafutia kipato ili kujikimu na familia zao
“Niwapongeze kwa ujenzi na kukamilisha kituo cha Polisi Sangambi na hatimaye Kimefunguliwa, lakini sasa naomba niwaombe wanaohusika kuendelea kuwaelimisha wananchi wa Kata hii juu ya matumizi sahihi ya Vyombo vya Moto jambo litakalofanya wananchi kuipenda huduma inayotolewa na kituo hicho” aliongeza Mhe Nshinshi
Awali akitoa taarifa za utekelezaji wa mradi huo Mtendaji wa kata ya Sangambi Bi Sarah Emmanuel amesema, Kata hiyo ilipokea shilingi milioni mia tatu ishirini na tisa na laki tano (329,500,000/=) kutoka Serikali kuu ili kutekeleza mradi huo huku akisema mpaka sasa ujenzi unaendelea vizuri kwa kushirikiana vyema na wananchi wa kata ya Sangambi kwa Ujumla wake
Diwani wa kata ya Sangambi Mhe Junjulu Ndete Muhewa wakati wa salamu zake za ukaribisho alisema Kata ya Sangambi haina mchezo katika usimamizi wa miradi ya Serikali, kwani utekelezaji wa miradi huwa shirikishi na wazi kwa wananchi wote jambo linalopelekea miradi inayotekelezwa katika kata hiyo kuwa bora zaidi
Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango imefanya ziara ya siku mbili, ni ziara ya kwanza tangu kuundwa kwa kamati mbalimbaliza Baraza la madiwani jambo linaloendelea kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli mbalimbali za Baraza la madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya na katika ziara yao wamepongeza na kushauri pale inapobidi

Bi Sarah Emmanuel Mtendaji wa Kata ya Sangambi akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Shule ya awali na msingi inayojengwa katika kata ya sangambi mbele ya Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya

Mhe Junjulu Ndete Muhewa Diowani wa kata ya Sangambi akitoa salamu za wananchi wa kata ya Sangambi kwa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wakati ilipotembelea mradi wa ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi inayojengwa kwenye eneo la Shule ya Sekondari Sangambi

Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Kelvin Nshinshi (Aliyeshika Karatasi) akiongoza Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi inayojengwa Sangambi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.