Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga ameongoza kamati ya usalama ya wilaya ya Chunya ikiamabatana na wakuu wa idara kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Chunya pamoja na viongozi kutoka taasisi mbalimbali kukagua miradi inayotaraji kupitiwa na mwenge wa Uhuru 2024 ndani ya wilaya ya Chunya
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 05/07/2024 ambapo miradi ya Elimu, Afya, Maji pamoja na maeneo mbalimbali yanayohusiana na mapokezi ya mwenge yamekaguliwa huku ushauri, maelekezo na maboresho yakitolewa na kamati ili kurahisisha zoezi la kukimbiza mwenge wa Uhuru utakapokuwa katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa wilayani Chunya tarehe 24/08/2024 hivyo wananchi mnaaswa kuendelea kujiandaa kushiriki katika zoezi hilo.
Mkuu wa wilaya ya Chunya (Aliyenyosha Mkono) akikagua mradi wa ujenzi wa madarasa shule ya Msingi Makongolosi (Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.