Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga ameongoza kamati ya Usalama ya wilaya ya Chunya ikiambatana na watalaam kukagua miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 utakapokimbizwa katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya. Ziara hiyo imefanyika leeo tarehe 12/06/2024
Mwenge wa Uhuru unataraji kupokelea tarehe 24/08/2024 katika kijiji cha Bitimanyanga kilichopo kata ya Mafyeko ukitokea Mkoani Tabora na baadaye kukimbizwa katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambapo utakagua miradi mbalimbali katika Nyanja za Elimu, Afya, Maji, Barabara na Miradi mingine mingi.
Mratibu wa Mwenge wilaya ya Chunya Ndu Simon Mbella (Aliyenyoosha Mkono) akifafanua Jambo eneo la uwanja ambapo Mwenge wa Uhuru utapokelewa wilayani Chunya
Mkuu wa wilaya ya Chunya (Aliyevaa shati la Draft) akizungumza na viongozi wa kijiji,kata pamoja na kamati ya usalama baada ya kukagua miundombinu mbalimbali eneo ambapo Mwenge wa uhuru utapokelewa
Mkuu wa wilaya ya Chunya akiiongoza kamati ya usalama pamoja na watalaam kukagua mradi wa ufugaji wa Nyuki Kipembawe, Pichani msafara ukipokea maelezo kuhusu mradi
Mkuu wa wilaya ya Chunya akiwa ameambatana na kamati ya usalama ya wilaya ya Chunya pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakikagua maendeleo ya ufungaji wa mashine katika kiwanga cha Kusindika Unga na Mafuta kinachojengwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Tumbaku (CHUTCU) ikiwa ni maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2024
Kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Chunya Mhandisi Burhan Nammanje akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Usalama wilaya ya Chunya baada ya kukagua ujenzi wa Daraja Lualaje
Mkuu wa wilaya ya Chunya akizungumza Jambo mbele ya Kamati ya usalama pamoja na watalaamu baada ya kukagua eneo ambapo mradi wa maji utatekelezwa katika kijiji cha Ifuma kilichopo kata ya Lupa mapema leo wakati wa ziara ya kamati ya usalama
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mtanda kilipochopo kata ya Mamba wakimsikilza Mkuu wa wilaya ya Chunya wakati wa ziara yake ya kutembelea kikundi cha vijana waendesha vyombo vya usafiri (Boda boda)
Mkuu wa wilaya ya Chunya akiiongoza kamati ya usalama pamoja na watalaamu kukagua mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Lola
Mkuu wa wilaya ya Chunya akiendelea kuiongoza Kamati ya usalama pamoja na watalaamu kukagua mradi wa ukarabati wa Shule ya Msingi Makongolosi ambapo Serikali ya awamu ya sita ilitoa shilingi milioni 90 ili kukarabati madarasa yaliyochokaa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.