WAJUMBE wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Machi 14, 2022 wamefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na mradi wa ujenzi kituo cha afya cha Sangambi unaokadiriwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 600, ambapo mapato ya ndani yalioyofanikisha mradi huo ni shilingi milioni 500 huku nguvu kazi za wananchi ikiwa ni shilingi milioni 100.
Kamati hiyo pia ilitembelea ujenzi wa soko la madini unaotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 497,430,119 ikiwa ni mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizungumza baada ya kukagua na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Abdallah Chaurembo ametoa pongezi kwa uongozi kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi.
“Tumetembelea kituo hiki cha afya, kizuri ujenzi wake unaendelea vizuri, tunawapongeza sana, lakini kituo hiki pamoja na kasi nzuri inayokwenda kwenye ujenzi tumeona ‘material’ (malighafi) yapo ya kutosha tunaamini kitaisha kwa wakati.” Alisema Chaurembo.
Chaurembo alisema kuwa, matumaini yake kwenye bajeti itakayopitishwa wiki ijayo, fedha zitatengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kituo cha afya ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha huduma za afya zinapatikanan kwa uhakika.
“Tunatarajia kwenye bajeti tunayokwenda kuijadili wiki ijayo tutaona fedha zimetengwa kwa ajili ya vifaa vya kituo hiki cha afya.” Alisema Chaurembo.
“Haitopendeza kituo hiki kimejengwa kwa gharama kubwa, wananchi wamejitolea na kamati ya Bunge na Mheshimiwa Mbunge amesisitiza tuje hapa, halafu tukaona kituo kinabaki majengo bila ya kutoa huduma.” Alionya Chaurembo.
Aidha, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wamemuagiza Meneja wa TARURA Mkoa kuhakikisha wanafanya matengenezo ya barabara ya Sangambi.
“Kutokana na umuhimu wa eneo hili Meneja wa TARURA tufanye kila inavyowezekana barabara hii iweze kufanyiwa matengenezo.
Tumeona uwekezaji mkubwa uliofanyika hapa halafu bila kuwa na barabara madhubuti ya kufika huku kituo hiki kinaweza kuwa kipo halafu hakifanyi kazi, sasa Meneja wa TARURA hili jambo mlichukulie umuhimu unaostahili.” Alisisitiza Chaurembo.
Kadhalika, Chaurembo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa kuaandaa taarifa nzuri.
“Nimepitia taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, nimeipitia kwa kina ambapo imeonesha mambo mengi humu ndani, naomba taarifa hii tuisome kwa kina na ikiwezekana Halmashauri nyingine zote pamoja na maelekezo tuliyoyasema yafanywe kama taarifa hii ilivyoandaliwa.”
Kwa upande wa Waziri wa Inchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa {TAMISEMI} Mhe. Innocent Bashungwa amewapongeza wananchi wa kata ya Sangambi kwa kuchangia nguvu kazi zao katika ujenzi wa miradi ya maendeleo.
“Pamoja na jitihada nzuri za Mweshimiwa Rais Samia Suluhu na Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza, nimefurahi kuona wananchi hapa hamjabweteka bado mnachangia shughuli za maendeleo.” Alisema Bashungwa.
Pia, Bashungwa ameutaka uongozi wa Mkoa kuzisimamia Halmashauri zote ili kuhakikisha matumizi ya fedha yanakuwa vizuri na kunakuwa na uwazi kwenye utumiaji wa fedha hizo.
“Ninachokielekeza hapa kwa Mkurugenzi na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa lisimamie hili kwenye halmashauri zote, fedha za Serikali zinazokuja kwenye maendeleo na zile fedha ambazo zinachangwa na wananchi kwa mapenzi yao kuchangia maendeleo kunakuwa na uwazi na uwajibikaji katika matumizi yake.” Alisema Mh. Bashungwa.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ua Utawala na Serikali za Mitaa wakipokea maeleozo ya Ujenzi wa Maradi wa Soko la Midini Unaotekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Chunya kupitia mapato ya Ndani
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakitembelea na Kukagua ujenzi wa kituo cha Afya cha Sangambi kilichopo kata ya Sangambi kinacho jengwa kwa Mapato wa Ndani
Muonekano wa Jengo la Wagonjwa wa Nje {OPD}
Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto pamoja na Wodi ya Wazazi, Kituo cha Afya Sangambi
Muonekano wa Soko la Madini linalijengwa na Halmashauri ya wilaya ya Chunya kupitia mapato ya Ndani
Muonekano wa Ndani Soko la Madini
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.