WAJUMBE wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Chunya katika kipindi cha robo ya tatu.
Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni ujenzi wa Vituo vya Afya vya Kambikatoo, Mafyeko, na Ifumbo pamoja na ujenzi wa Zahanati ya Lyeselo na Igangwe.
Pia kamati ilitembelea na kukagua ujenzi wa majengo manne katika Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa jengo la Bohari ya Dawa, ujenzi wa Jengo la Upasuaji pamoja na ujenzi wa Wodi ya Wanawake na Wanaume.
Akiongoza wajumbe wa Kamati hiyo Mheshimiwa Bosco Mwanginde ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ameupongeza uongozi wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa Wilayani Chunya.
“Mimi binafsi na kwa niaba ya wajumbe wenzangu niwapongeze kwa hatua mliyofikia, mara ya kwanza nilikuja hapa nikakuta pori lakini leo tunaona mpo hatua nzuri za ukamilishaji.
“Nampongeza Mkurugenzi wetu na wataalamu wake kwa ufuatiliaji wao kwenye ujenzi wa miradi ndani ya Halmashauri yetu nawaomba waongeze bidii ili miradi yote ikamilike kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi wetu.” Alisema Mwanginde.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Lualaje ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Mheshimiwa Tusalimu Mwaijande ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi kwa jitihada wanazozifanya hadi sasa za kupeleka maendeleo kwa wananchi.
“Niipongeze Ofisi ya Mkurugenzi kwa namna ambavyo wanakimbiza hii miradi kwa ujumla, wataalam wetu wanafanya kazi nzuri sana kufuatilia miradi hii na kuhakikisha fedha iliyopelekwa kwenye mradi inafanya kazi iliyokusudiwa.” Alisema Mwaijande.
Aidha, kamati pamoja na kutoa pongezi na kuridhishwa na mwenendo wa miradi ya maendeleo wameagiza miradi yote ya maendeleo kukamilika kwa wakati ili ilete tija na maendeleo kwa wananchi huku ikisimamiwa katika ubora stahiki na kwa weledi mkubwa.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wakikagua Ujenzi wa Kituo cha Afya Ifumbo
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Wakitembelea na Kukagua Ujenzi wa Jengo la Utawala
Muonekano wa Jengo la Utawala
Wajumbe wa Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango wakikagua ujenzi wa Nyumba ya Wtumishi 3 in 1 katika kituo cha Afya cha Kambikatoto
Muonekano wa nyumba ya Watumishi ya 3 in 1 Katika kituo cha afya cha Kambkatoto
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.