Kamati ya kudumu ya madiwani ya fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde imewataka watoa huduma ya Afya katika zahanati ya Everest kutoa huduma bora na zinazokidhi matarajio ya wananchi.
Wito huo umetolewa na kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya chunya Mhe Mwanginde wakati wa ziara ya kamati ya fedha uongozi na Mipango wakitembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne 2022/2023.
“Sisi chunya tuna changamoto ya huduma ya afya tunazo zahanati za serikali lakini watu hawazitumii sana wakiamanini kwamba kunakuwa hakuna dawa, hakuna wataalamlu wazuri, nyie mmeanzisha tunaamini ni wataalamu na mpo eneo sahihi na lina watu wengi huduma zenu zitawafanya mpate wateja wengi angalieni sana huduma kuanzia mapokezi na namna ya kuwatibu watu” alisema Mwanginde
Kmati hiyo iliongeza kuwa wananchi wanategemea huduma bora wanapofika kwenye zahanati kupata huduma za afya hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanatoa huduma bora na stahiki kwa wananchi wanaofika kupata huduma katika zahanati hiyo.
“Jitahidini sana kutoa huduma bora ambayo itawavutia na kuwashawishi wananchi waje hapa kupata huduma na ndipo mtaona mafanikio” alisema Mhe. Mwanginde
Aidha kamati imewapongeza wanakikundi hao kwa wazo la kuanzisha zahanati hiyo na imewataka kuhakikisha wanatoa huduma za kizahanati na sio kulazimisha kutoa huduma zisizo za kizahanati.
Katika hatua nyingine kamati imewapongeza wataalamu wa hamashauri ya wilaya ya Chunya kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi inayoendelea kutekelezwa ndani ya wilaya.
Kamati imetembelea na kukagua miradi mbalimbal ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya wilaya ya chunya kwa upande wa sekta ya Afya miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa jingo la wagonjwa wan je (OPD) na ujenzi wa Wodi ya grade one katika Hospitali ya wilaya ya Chunya, Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi, imetembelea Kikundi cha vijana cha UPENDO DISPENSARY GROUP kilichopo kata ya Chokaa ndicho mmliki wa Zahanati ya Everest baada ya kunufaika na mikopo inayotolewa na halmashauri.
.
Kwa sekta ya elimu miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni Ujenzi wa vyumba vya madarasa 2 katika shule ya Msingi mapogolo, ujenzi wa Shue mpya ya Msingi Nyerere katika kata ya makongolosi sambamba na Ujenzi wa shule mpya ya Msingi Mafyeko kata ya mafyeko zinazotekelezwa kupitia mradi wa Boost.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.