.Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhe.Suma Fyandomo amewataka wanawake kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi KWANI UWEZO wanao na hawashindwi kutekeleza majukumu mbalimbali ya Kifamilia, Kijamii na kitaifa kwa ujumla huku akisistiza kuondoa hofu wakati wa kutina ya kufanya jambo lolote
Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 05 Machi 2024 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani kiwilaya yaliyofanyika katika viwanja vya Msifuni kijiji cha Ifuma kata ya Lupa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake kiwilaya .
“Wanawake niwatie moyo kwenye nafasi zozote zinapojitokeza msisite, msiogope mnatakiwa kusonga mbele kuwa mstari wa kwanza kwenda kuchukua fomu au kuomba nafasi hizo kwasababu wanawake tunaamini hatushindwi , wanawake ni Jeshi kubwa lakini pia ni nguzo kubwa ya familia”amesema Mhe. Fyandomo.
Aidha Fyandomo ameongeza kuwa wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza mbele yao akisema ujasiri ndio iwe nguvu ya kuchangamkia fursa hizo kwani uwezo wanao na wanaweza hata wasipowezeshwa huku akirejerea uwezo wa wanawake kukabili majukumu ya Familia zao pindi wakinababa wa familia wanapokuwa wametelekeza familia zao
“Nitumie jukwaa hili kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hasaani kwa kuuvaa Ujasiri wa hali ya juu kuongoza Royal tour ambayo imezaa matunda, watalii wameongezeka lakini pia imetuingizia fedha za kigeni ambazo zimesadia katika kukuza uchumi wetu”alisema Fyandomo.
Akisoma risala kwa Mgeni rasmi katibu wa kamati ya maandalizi ya siku ya Wanawake duniani wilaya ya Chunya Bi Bahati Mwampetele amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imefanya jitihada mbalimbali katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya biashara , kwendelea kutoa elimu kwa jamii kupinga vitendo vya ukatili , kutoa elimu ya malezi na makuzi ili kuwajengea wanawake uwezo wa kujiamini.
Maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi ambapo kwa Wilaya ya Chunya Maadhimisho hayo yamefanyika leo tarehe 05 Machi 2024, yakienda sambamba na ugawaji wa vifaa mbalimbali kama vile viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu, vifaa vya usafi kituo cha Afya cha Lupatingatinga, fedha pamoja na vitu vingine kwa wahitaji
Mhe.Suma Fyandomo alieshika maiki Mbunge viti Maalum akizungumza neno baada ya kukabidhi viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu wakati wa maadhimisho ya sikuya wanawake duniani yaliyoadhimisha kiwilaya katika kata ya Lupa kijiji cha Ifuma.
Wanachama wa TALGWU wakiwa wamebeba baadhi ya vifaa vya usafi kwaajili ya kukabidhi katika kituo cha Afya cha Lupatingatinga ikiwa ni sehemu ya vitu vilivyofanyika katika siku ya maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika kiwilaya katika kata ya Lupa
Mhe. Fyandomo Mbunge viti maalum Mkoa wa Mbeya aliye vaa gauni lenye rangi ya blue akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake walipotembelea kituo cha Afya cha Lupatinatinga kwaajili ya kuwaona Wagonjwa nakugawa vifaa vya Usafi
Mhe.Masache Kasake Mbunge wa jimbo la Lupa akicheza pamoja na wanawake wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kiwilaya katika kata ya Lupa kijiji cha Ifuma.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.