John Felix Maholani mwenyekiti katika kikao cha kamati ya lishe akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chunya amemtaka Kaimu Afisa elimu awali na msingi ndugu John Daniel Gwimile kuhakikisha wanakuwa na takwimu sahihi zinazoonyesha ni watoto wangapi wanapata chukula cha mchana shuleni na wangapi hawapati chakula shuleni ikiwa ni utaratibu wa kuhakikisha watoto wote wanapata chakula cha mchana shuleni .
Ametoa kauli hiyo julai 19/07/2023 wakati wa kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halimashauri ya wilaya ya Chunya ambacho hufanyika kila robo mwaka kwaajili ya kutoa tathimini ya hali ya lishe kiwilaya.
‘’Kaimu afisa elimu awali na msingi mjitahidi kuhakikisha mnapata takwimu sahihi zinazoonyesha idadi ya wanafunzi wanaochangia na kupata chakula shuleni na idadi kamili ya wanafunzi ambao hawachangii na hawapati chakula cha mchana shuleni’’
Akisoma taarifa ya tathimini ya lishe ya robo mwaka ya kuanzia mwezi april hadi juni kaimu Afisa Lishe wilaya ya Chunya Ndugu Witness Kisukulu amesema idara ya afya inawajibu wa kuhakikisha jamii inatumia chumvi zenye madini joto kwa kupima chumvi hzo ili kuzuia ugonjwa wa goita ,ameongeza kuwa kumekua na changamoto ya baadhi ya wanafunzi kutokula chakula cha mchana shuleni kutokana na baadhi ya wazazi kuto changia mchango wa chakula utakao mwezesha mtoto kupata chakula cha mchana anapokuwa shuleni .
Kaimu Afisa maendeleo ya jamii Ndugu Ester Kondobole amesema kuwa elimu ya lishe imekuwa ikitolewa katika vikundi mbalimbali, wakina mama wajawazito na wanaonyonyesha lakini pia kwa wanufaika wa mradi wa kunusuru kaya masikini (TASAF) ili kuhakikisha hali ya lishe inaimarika na jamii inaepukana na udumavu
‘’Tumeendelea kuwajerngea uwezo wawezeshaji wa wanaotoa elimu kwa wanlengwa wa TASAF juu ya masuala ya lishe ambapo jumla ya wajumbe 26 kutoka katika kata 20 wamepewa mafunzo ya lishe , lakini pia tumeendelea kutoa elimu hiyo katika vikundi vya ujasiriamali vyenye jumala ya wajumbe
Naye afisa kilimo na mifugo ndugu Paul Lugodisha amesema kuwa idara imeendelea kuhamasisha jamii kulima vyakula vya msimu kama buustani za mbogamboga kwa msimu huu wa kiangazi lakini sambamba na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya viwatilifu vya kuhifadhia chakula na kuendeea na ukaguzi wa wanyama ili kumrinda mtumiaji
Lakini pia afisa elimu msingi amesema kuwa wameendelea kuhamasisha ukusanyaji wa chakula wakati wa mavuno shuleni ili kuhakkisha watoto wanapata chakula cha mchana wanapokuwa shuleni kwa kuhamasisha wazazi kuchangia chakula pamoja na na kuhakikisha kila shule inakuwa na shamba darasa ili kupunguza uhaba wa chakula shuleni
Kikao hiki ni mwendelezo wa vikao vingine vya tathimni vinavyofanyika kila robo mwaka ikiwa ni kikao cha robo ya nne (4) kinacholenga kutoa tahimini ya hali ya lishe katika halmashauri ya wilaya ya chunya kikihusisha wataalamu kutoka katika idara mbalimbali suala la lishe ni swala mtambuka ambapo idara mbalimbali zimetoa tarifa zinazohusu utekelezaji wa masuala ya lishe ikiwa ni pamoja na idara ya kilimo na mifugo, Idara ya maendeleo ya jamii ,Idara ya elimu msingi, Idara ya elimu sekondari na idara zingine.
kaimu Afisa Lishe wilaya ya Chunya Ndugu Witness Kisukulu akitoa Taarifa Mbele ya Kikao cha Tathimini ya lishe Robo ya nne ya mwaka 2022/2023
Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya ambaye ndiye Katibu wa Kikao cha Lishe Dkt Darson Adrew akizungumza na kufafanua jambo Mbele ya Mwenyekiti na wajumbe wa kikao
Kaimu afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Chunya Ndugu Ester Kondobole akichangia mjadala katika kikao cha Lishe kwa Robo ya nne 2022/2023
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Lishe wakiendelea na mijadala mbalimbali ili kutathimini maendeleo ya Lishe katika Halmsahuri ya wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.