Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya Dkt Stephen Mwakajumilo amewataka wakuu wa shule za sekondari Mkoa wa Mbeya kujitafakari kama wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwani walimu ni msingi imara na muhimu wa Maendeleo ya Taifa lolote Duniani
Dkt Mwakajumilo ametoa kauli hiyo leo tarehe 26/5/2023 kwenye kikao cha wakuu wa Shule Mkoa wa Mbeya (TAHOSA) kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) chenye lengo la kukumbushana, kuhimizana na kubadirisha uzoefu na ujuzi ili kuleta ufanisi wa wakuu wa shule katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwenye maeneo ya kazi
“Elimu mliyopata miaka ya nyuma haitoshi lazima muingie mifukoni ili kuitafuta Elimu itakayowafanya mpambane na maendeleo ya sayansi na teknolojia tuliyonayo sasa na muungane muwe kitu kimoja na muiambie serikali changamoto zetu ili kunusuru kizazi cha sasa maana bila walimu hakuna Taifa. Msikubali Elimu zenu zioze, bali zifanyieni kazi, hakikisheni mnatafuta maarifa mengine ili kuweza kutatua changamoto zinazoambatana na maendeleo ya sayansi na Teknolojia” Mwakajumilo
Akijibu hoja ya walimu kutaka siku za kumfukuza Mwanafunzi mtoro zipunguzwe Dkt Mwakajumilo amewataka walimu kuwa karibu na wanafunzi ili kutambua changamoto zao mapema kwani sio wote wanaoshindwa kufika shule kwasababu ya utoro tu bali ni changamoto mbalimbali
“Usikubali kumpoteza mwanafunzi wako, usikubali kumfanya mwanafunzi wako kuwa adui, bali mfanye awe rafiki yako ili aendelee kupenda masomo wakati wote na hii inaweza kusaidia hata kupunguza utoro wa wanafunzi shuleni” amesema Mwakajumilo
Awali akisoma Risala kwa Mgeni rasmi Mwenyekiti wa wakuu wa shule za sekondari Mkoa wa Mbeya Mwalim Francis J. Mwakihaba ameomba kupunguzwa kwa siku za kumfukuza mwanafunzi mtoro shuleni kutoka siku tisini (90) na kufikia thelasini (30) ili walimu waweze kukomesha suala la utoro kwa wanafunzi
“Sisi wakuu wa shule tunaomba idadi za siku za mwanafunzi mtoro kufukuzwa shule zipunguzwe kuto tisini (90) kama ilivyo sasa na kufikia siku thelesini (30) jambo ambalo litapelekea walimu wakuu na uongozi wa shule kuwaondoa wanafunzi watoro kwa wakati ili kuleta ufanisi na ufaulu katika masomo, kwani kuna wanafunzi wanakuwa watoro kwa siku themanini (80) na baadaye anaruhusiwa kufanya mitihani wakati hajafanya maandalizi” Mwl. Mwakihaba
Akitoa shukrani kwa mgeni rasmi Mwalimu Mulla O. Njeje pamoja na kumshukuru mgeni rasmi kufika wilaya ya Chunya pia amemuhakikishia kwamba ujumbe alioutoa umefika eneo sahihi na pia kwa niaba ya walimu wakuu wote Mkoa wa Mbeya, Mwalimu Njeje amemuhakikishia Mgeni Rasmi kwamba ujumbe alioutoa utawafikia walimu wote
“Mimi naamini haya uliyotupatia tutayapeleka kwa walimu wenzetu na hata yale yanayohitaji utekelezaji tutayatekeleza ipasavyo hivyo maneno yako yamefika maeneo sahihi kabisa” amesema Mwl. Njeje
Kikao hiki ni kiako cha kawadaida na Kimefanyika wilayani Chunya ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa vikao hivyo kukaa kwa kubadirishana wilaya moja hadi nyingine zilizopo Mkoani Mbeya hivyo kwa sasa ilikuwa ni nafasi ya wilaya ya Chunya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.