Naibu waziri wa Madini Dkt Steven Kiluswa amewataka wachimbaji wanaotorosha madini kuacha mara moja kwani kutorosha madini ni kukosa uzalendo kwa nchi yako ili hali sekta ya madini imeboreshwa kwa kiwango kikubwa kwani masoko ya madini yameanzishwa nchini na vituo vya kununulia dhahau vinapatikana karibu kila kona
Mhe. Kiluswa amesema hayo leo tarehe 15/03/2023 alipokuwa anazungumza katika hafla ya ufunguzi wa maonesho ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika mkoa wa kimadini Chunya, maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Sinjilili ambapo taasisi mbalimbali binafsi na serikali zinashiriki pamoja na wachimbaji wadogo na wakubwa kutoka katika mkoa wa kimadini Chunya na hata nje ya mkoa huo
“Serikali imeweza kuanzisha masoko 52 ya madini, vituo 92 vya ununuzi wa madini na uwepo wa masoko haya umepunguza utoroshaji wa madini. Watoroshaji wa madini acheni kutorosha madini kwana hamna sababu ya kufanya hivyo maana masoko yapo na kuendelea kufanya hivyo ni kukosa uzalendo, na serikali iko macho kuhakikisha madini hayaendelei kutoroshwa” amesema Dkt Kiluswa
Aidha Dkt Kiluswa ameshauri mkoa wa kimadini Chunya Kuendelea kuwa na maonesho kama haya kwani yana mchango mkubwa sana katika kufungua fursa mbalimbali katika maeneo ya uchimbaji na Nyanja nyingine za kiuchumi kwani huwakutanisha wachimbaji, brokers, Dealers na wadau wengine wengi ambao huduma zao zinafanikisha mchakato wote wa uchimbaji
“Muwe na siku ya madini angalau kwa kila mwaka ambapo teknolojia mbalimbali zinaoneshwa hapo ili kuendelea kufungua fursa mbalimbali za uwekezaji kwani hata kupitia maonesho haya wako watu watakuja kuwekeza chunya kwani fursa hizo wameziona kupitia maonesho haya. Kongamano kama hili litatuwezesha kuwakutanisha wachimbaji wa madini kutoka maeneo mbalimbali, brokers, dealers na watoa huduma mbalimbali zinazohitajika katika mchakato wa uchimbaji”
Awali wakati Mgeni Rasmi anatembelea mabadna mbalimbali ya wadau waliojitokeza, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera ameziomba taasisi za kifedha kupunguza Riba kwa wachimbaji angalau kufikia asilimia kumi na moja ili kuendelea kuwarahisishia katika shughuli zao tofauti na ilivyosasa ambapo wachimbaji hukopeshwa kwa riba ya asilimia ishirini
“Riba naomba mshushe angalau mpaka asilimia kumi na moja ili angalau waweze kujikwamua na hii imekuwa changamoto kubwa kwao, riba hii ikifika asilimia kumi na moja mimi nitafarijika sana” alisema Homera
Sekta ya madini kwa sasa inachangaia asilimia 9.7 katika pato la Taifa ambapo Ilani Ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ikielekeza ifikapo 2025 sekta ya madini ifikishe asimilia kumi (10%) katika pato la Taifa huku ajira zinazozalishwa kutoka na sekta ya madini nchini mpaka sasa ni Milioni nane
Maonesho ya kwanza ya teknolojia ya Madini na fursa za uwekezaji mkoani Mbeya yamefunguliwa rasmi leo terehe 15 march na Naibu waziri wa madini Dkt Steven Kiluswa katika viwanja vya Chunya kati vilivyopo kata ya Itewe kijiji cha Sinjilili wilayani Chunya ambapo kauli mbiu ya maonesho hayo ikiwa ni “Uongezaji wa thamani na Madini kwa maendeleo ya Taifa”. Maonesho hayo yatadumu mpaka tarehe 17/3/2023.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.