Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Tamimu Kambona akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chunya amewataka wananchi kushirikiana kwa pamoja kuwafichua watu wanaotenda matendo ya ukatili katika jamii zetu ili waweze kuchukuliwa hatua kwani kwa kufanya hivyo matendo ya ukatili yatapungua na jamii itabaki salama na kuwataka wasikae kimya wanapoona mtu kafanya vitendo vya ukatili.
Kauli hiyo ametoa leo Desemba 10, 2023 wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsi yaliyofanyika katika kijiji cha Shoga kata ya Sangambi ambapo wilaya ya Chunya aimehitimisha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia
“Ndugu wananchi ni jukumu la kila mmoja wetu kupinga vitendo vya ukatili hivyo tunapaswa kushirikiana kwa pamoja kutokomeza vitendo vya ukatili lakini pia kama mzazi umeona mwenzio anamfanyia mtoto vitendo vya ukatili na ukakaa kimya vitendo vya ukatili havitakoma hivyo tuwafichue wale wote wanaofanya vitendo vya ukatili katika jamii zetu tusikae na adui jirani” alisema Kambona
Aidha Kambona amekea wakina baba wanaotoroka majukumu yao ya msingi jambo linalopelekea wakina mama kuwa na mziko mzito wa majukumu jambo linalopelekea ukatikli wa kijinsia kwao
“Wanawake na wasichana ndio kundi linalopitia changamoto nyingi kutokana na mgawanyo wa majukumu ya kifamilia akinababa tumekuwa tukikwepa majukumu mengi ambayo mengine tungeweza kuyafanya ndani ya familia mfano ndani ya familia tumevuna mazao baba anaamua kuyachukua na kwenda kuyauza na kumwacha mama anahangaika na familia” alisema Kambona.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Dkt Darison Andrew amesema madhara ya ukatili ni makubwa na yanagharama kubwa ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha au kupata maradhi hususani kwa mtu aliefanyiwa ukatili wa kingono, ukeketwaji na aina nyingine za ukatili hivyo jamii inapaswa kupinga vikali vitendo vya ukatili.
Awali akisoma risala kwa Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa jamii wilaya ya Chunya Bi Lightness Mbissa amesema miongoni mwa changomoto zinazowakabili ni pamoja na wazazi na walezi kumalizana nyumbani wao kwa wao pindi matukio ya kikatili yanapokuwa yametendeka pasipo kufikishwa katika vyombo husika hali inayochangia kwa kiasi kikubwa matukio ya ukatili wa kijinsia kuongezeka katika jamii.
Kwa niaba ya wazee wa wilaya ya Chunya Mzee Mosses Zumba amesema wazee wanapaswa kukemea vitendo viovu vinavyoendelea katika jamii hasa ukatili wa kijinsia kwani wazee wana nafasi kubwa katika jamii hivyo wanapaswa kutengeneza utaratibu wa kukaa na kuongelea na kupinga vitendo vya kikatili
Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia imetamatika leo ambapo wilaya ya Chunya imehitisha katika kijiji cha Shoga kilichopo kata ya sangambi, katika kipindi cha siku kumi na sita wananchi 1029 wamefikiwa wanaume ikiwa ni 422 na wanawake 607 huku elimu mbalimbali ikitolewa kama vile elimu ya kujitambua, elimu ya ukatili na mambo mengine mengi
Wananchi wa kijiji cha Shoga wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kilele cha kampeniya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoyofanyika kijijini hapo
Mganga Mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya Dr Darison Andrew akielezea madhara ya Ukatili katika jamii wakati wa kilele cha kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kijiji cha Shoga.
Mzee maarufu ndugu Mosses Zumba akiongeajuu ya umuhimu wa wazee katika kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii wakati wa kilele cha kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kijiji cha Shoga
Mwenye kiti wa jumuiya ya wazazi kupitia chama cha Mapinduzi ( CCM) akitoa neno la shukurani kwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Shoga
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.