Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona amewataka wananchi wa Chunya hasa walengwa wa TASAF kuendelea kuibua miradi yenye tija na manufaa kwao na Jamii kwa ujumla huku akiwataka kuendelea kujituma katika kufanya kazi zao za kujipatia kipato ili kuwa na maisha bora.
Ametoa kauli hiyo mapema leo 16.07.2025 wakati alipotembelea miradi mbalimbali iliyoibuliwa na walengwa wa TASAF ili kutatua baadhi ya changamoto zinazoikumba jamii ya eneo fulani ambapo amesema kupitia miradi hiyo ufumbuzi wa changamoto mbalimbali umepatikana kupitia miradi hiyo.
“Kwanza kabisa hongereni kwa miradi hii mnayoendelea kutekeleza, tumepita baadhi ya maeneo wamefungua barabara, wengine miradi ya maji na hatimaye na ninyi hapa mna mradi wa visima vya maji, Napongeza sana, Muendelee kushirikiana na Serikali kuibua Miradi yenye tija na yenye manufaa kwenu na Jamii kwa ujumla” Amesema Kambona.
Aidha, Kambona amempongeza Mratibu wa TASAF Halmashauri ya wilaya ya Chunya pamoja na timu nzima kwa usimamizi, bidii na kujituma kwao katika kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo huku akisema utekelezaji mzuri wa miradi unatokana na usimamizi mzuri.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu David Ngowo amesema walengwa wa TASAF katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya wamekuwa wakiibua miradi wao wenyewe na wakiitekeleza jambo linalosaidia kuondoa baadhi ya changamoto katika maeneo yao huku akirejerea maeneo ambayo hayakuwa na barabara kupitia TASAF barabara zimepatikana, maeneo ambayo hayakuwa na maji sasa kupitia TASAF mmepata maji changamoto nyinginezo.
Mhandisi wa Halmashauri ya Chunya Eng. Sophia Mgaya na Afisa Mipango na uratibu walioongoza na Mkurugenzi kwenye ziara hiyo wametoa ushauri maeneo mbalimbali ili wananchi wa Chunya waendelee kutekeleza miradi yao kwa viwango stahiki ili iweze kudumu kwa muda mrefu na iendelee kuwasaidia wananchi kwa muda mrefu zaidi.
Miradi iliyotembelewa leo ni mradi wa ujenzi wa Barabara kijiji cha Mbugani, Mapogoro, Makongolosi, kijiji cha Upendo, Lola, Mtande na Mamba huku mradi wa maji Gepu, na mradi wa Lambo la maji Makongolosi unaounganisha na upandaji wa miti kuzunguka lambo la maji.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona (Aliyevaa Tisheti Nyeupe Katikati na amenyoosha mkono) akitembelea mradi wa Barabara ilifunguliwa na Walengwa wa TASAF kijiji cha Mbugani, Kulia kwake ni Mratibu wa TASAF Chunya na Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbugani
Mkurugenzi mtendaji (Mwenye tisheti Nyeupe) akipokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa lambo la maji Makongolosi, Mradi huo umeambatana na upandaji wa miti kuzunguka lambo hilo
Mkurugenzi mtendaji akipokea taarifa ya uchimaji wa kisima cha maji Gepu uliotekelezwa na walengwa wa TASAF ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo
Mratibu wa TASAF wilaya ya Chunya Ndugu David Ngowo (Aliye nyoosha mkono wenye makaratasi) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi mtendaji wakati wa ukaguzi wa mradi wa Barabara katika kijiji cha Lola kilichopo kata ya Upendo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.