Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S.Mayeka amesema kuwa wazazi na walezi wanajukum kubwa la kuhakikisha wanashiriki vyema katika malezi kwa kufuata na kuzingatia masuala mbalimbali ya lishe yanayotolewa na wataalam ili kuiwezesha halmashauri kushika nafasi ya kwanza kwani imekuwa ikishika nafasi ya tatu mfululizo.
Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 31/10/2023 wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa ambapo kiwilaya yameadhimishwa katika viwanja vya shule ya Msingi Mlimanjiwa iliyopo kata ya Mbugani wilayani Chunya.
‘’Nafasi ya tatu tumeizoea sasa tunataka nafasi ya kwanza niwaombe wazai, walezi na watoto mwendelee kusikliza na kufuata maelekezo ya wataalamu tulishika nafasi ya tatu kwasababu mlisikiliza na kufuata maelekezo ya wataalamu hivyo hata kushika nafasi ya kwanza itawezekana kama mtasikiliza na kufuatilia maelekezo yote mnayopewa na wataalamu.’’alisema Mhe. Mayeka.
Aidha amempongeza Mkurugenzi mtendaji , idara ya afya pamoja na idara zote zinazohusika na masuala ya lishe kwa juhudi kubwa ambazo wamekuwa wakizifanya ikiwa ni pamoja na kutenga bajeti kubwa kwaajili ya kufanikisha masuala ya lishe lakini pia kuhakikisha watoto wanapata chakula wanapokuwa mashuleni.
Akitoa salam katika maadhimisho hayo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilya ya Chunya ndugu Tamim Kambona amemuhakikishia mkuu wa Wilaya ya chunya kuwa uwezekano wa kushika nafazi ya kwanza upo kwani idara mbambali za halmashauri zimepewa majukumu ya kutekeleza katika masuala ya lishe ikiwepo idara ya kilimo kwa kutengewa bajeti ili kuhakikisha mazao mbalimbali ya lishe yanalimwa na kutumiwa na wananchi ili kuboresha afya zao .
"lengo letu kama halmashauri ni kutoka kwenye nafasi ya tatu, ya pili na kushika nafasi ya kwanza kwani uwezo wa kufanya hivyo Mhe. Mkuu wa Wilaya tunao ni sisi kuamua na kujipanga kuhakkikisha yale yote yaliyoko kwenye bajeti zetu yanatekelezeka na hatimaye tuweza kufikia lengo la kushika nafasi ya kwanza katika masuala ya lishe” alisema Mkurugenzi.
Akimwakilisha Mgaga Mkuu wa Wilaya Daktari Edward Tengulaga Mfamasia wa wilaya ya Chunya amesema kuwa lengo la kampeni ya lishe kwa Vijana rika balehe ni kunusuru vijana rika balehe kwa kutoa elimu ya lishe kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika ambazozinaonyesha kuwa hali duni ya lishe inaanzia mashuleni na kizaki kinachoathirika sana na lishe duni ni kizazi rika balehe.
‘’Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imefanya kampeni ya lishe kwa vijana rika balehe katika Shule za Sekondari Isenyela , Kiwanja na Itewe Sekondari ambapo jumla ya vijana rika balehe 945 walipimwa hali ya lishae, wanafunzi wa kike 588 wanafunzi wa kiume 365 na kubaini wanafuzi 87 walikuwa na uzito uliozidi na wanafunzi 13 walionekana kuwa na ukondefu’’alisema Tengulaga
Maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa huadhimishwa kila mwaka mwezi Oktoba, kwa mwaka 2023/2024 maadhimisho haya yameadhimishwa leo 31/10/2023 yakioongozwa na kauli mbiu ‘’Lishe bora kwa Vijana Balehe, Chachu ya Mafanikio yao” ambapo wilaya ya Chunya imetumia viwanja vya shule ya msingi Mlimanjiwa kuadhimisha siku la Lishe Kitaifa ambapo yamekuhudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Chunya, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Mkurugenzi mtendaji na wataalam mbalimbali kutoka halmashauri , wananchi pamoja na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.
Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu Kambona akitoa salamu Mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya wakati wa Maadhimisho ya siku ya Lishe yaliyofanyika viwanja vya shule ya msingi Mlimanjiwa
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya Dkt Edward Tengulaga akitoa salamu na mwenendo wa Lishe wilaya ya Chunya wakati wa Maadhimisho ya siku ya Lishe mwaka 2023 katika viwanja vya shule ya msingi Mlimanjiwa
Mkuu wa wilaya ya Chunya akimkabidhi cheti cha kufanya vizuri katika mkataba wa Lishe Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mlima Njiwa mw. Asajile Juma Ndiga wakati wa Maadhimisho ya siku ya Lishe
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Isenyela wakishiriki Mchezo wa Kuvuta kamba kati ya Timu yenye Lishe bora na Timu yenye lishe Duni wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.