Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka Simon Mayeka amewataka maafisa ugani na kilimo wilayani chunya kuwaelimisha wananchi kutunza Chakula ili kuepuka changamoto za kukosekana kwa chakula mwaka ujao jambo linaloweza kupelekea kushuka kwa uzalishaji na Nguvukazi kwa ujumla.
Mhe. Mayeka amesema hayo leo wakati akikabidhi pikipiki kwa maafisa ugani na kilimo wilayani chunya ikiwa ni mwendelezo wa zoaezi la ugawaji wa pikipiki kwa maafisa ugani, maafisa kilimo pamoja na watnedaji wa kata nchi, ambapo pikipiki 33 zimegawiwa kwa maafisa ugani na maafisa kilimo wilayani chunya
Mhe. Mayeka amewataka maafisa ugani na maafisa kilimo wilayani humo kuhakikisha wanatumia vitendea kazi hivyo kuwafikia wakulima kutatua changamoto zianzowakabili na baadaye kuleta tija katika familia na Taifa kwa ujumla
“Inawezekana tukavuna vizuri sana mwaka huu kutokana na mwenendo wa mvua lakini muhimu sana wakulima wasisitizwe kutunza chakula kwani maeneo mengine nchini na nje ya nchi hali sio nzuri, hivyo kupitia vitendea kazi hivi nendeni mkatusaidie kuhimiza wakulima kutunza chakula kwaajili ya matumizi yao hapo baadaye”
Aidha Mhe. Mayeka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anasaidia kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya kila siku kwa watumishi wake, sisi kazi yetu ni kumlipa kwa kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi
“Nimshukuru sana Mhe. Rais kwa namna anavyotusaidia kutekeleza majukumu yetu kwa kutupatia vifaa hivi, Hivyo Rais ametiza wajibu wake, wizara imetimiza wajibu wake, eneo lililobaki ni lako wewe. Hatutegemei uzembe wowote utajitokeza kwako, hivyo tunakutarajia wewe kuhakikisha wakulima na wafugaji wananufaika na hatimaye Taifa kwa ujumla wake”
Awali wakati akimkaribisha Mkuu wa wilaya ya Chunya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Ramadhan Shumbi ambaye ni Diwani wa kata ya Mamba amewataka maafisa ugani na maafisa kilimo hao kuhakikisha tija ya kupewa vifaa hivyo inaonekana kupitia kazi
“Mmepewa vitendea kazi hivi ambavyo mkuu wa wilaya atakabidhi muda mchache ujao, nawaomba kazi ikafanyike kwani wako wakulima wanalima eneo kubwa na mapato ni kidogo hivyo kupitia vitendea kazi hivi mzunguke kutoa elimu ya kilimo ili wapate tija mfanye hivyo na kwa wafugaji pia” amesema Mhe Shumbi
Kwaniaba ya Maafisa ugani na Maafisa kilimo walipokea pikipiki hizo, Afisa kilimo Felis Mendrad kutoka kata ya Mamba na Msafiri Sufiani Magasa afisa ugani kata ya Mbugani kwa pamoja wameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa vifaa hivyo na pia wamemshukuru Mkuu wa wilaya ya Chunya kwa kuwakabidhi vifaa hivyo na wameahidi kuvitumia kama maelekezo yanavyoeleza na lengo kubwa ikiwa ni kuleta tija kwa wakulima na wafugaji katika maeneo yao ya kazi
Jumla ya pikipiki 33 zimegawiwa leo ambapo pikipiki 27 zimegaiwa kwa maafisa kilimo na maafisa ugani wakati pikipiki 6 zimegawiwa kwa maafisa watendaji wa kata.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka akimkabidhi pikipiki Bi. Felis Mendrad Afisa Ugani wa kata ya Mamba
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.