MKUU wa Wilaya ya Chunya Mh Mayeka Simon Mayeka ametoa wito kwa wakazi wote wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi la ubainishaji wa barabara za Mitaa.
Mayeka ameyasema hayo wakati wa zoezi la ubainishaji wa barabara za MitaaAprili 21, 2022 kwa kuweka vibao vya maelekezo katika barabara ya Mapogoro.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uwekaji wa vibao vya maelezo ya mitaa na namba kwenye nyumba, Mh.Mayeka amesema uzinduzi wa barabara ya Mtaa wa Mapogoro katika Wilaya ya Chunya unawakilisha mitaa yote ya Wilaya hiyo, akibainisha kuwa mfumo wa Anuani za Makazi utasaidia kurahisisha upatikanaji wahuduma mbalimbali za kijamii.
“Awaliyayote niwapongeze kwa zoezi hili,tumeanza kuweka vibao vinavyoonesha majina ya mitaa zoezi hili litakuwa endelevu kwa wilaya nzima, barabara zetu zote zitawekewa vibao vya utambulisho” amesemaMhMayeka.
Aidha Mayeka amekemea vikali wananchi ambao wataku wananiaovu ya kutakakung’oa vibao hivyo kwa manufaa yao wenyewe.
“Vibao hivi nikwamanufaa ya wananchi wote, kuna wananchi wachache wabinafsi ambao wao wanaangalia faida yao, watataka kung’oa vibao hivi na kwenda kuuza kwenye vyuma chakavu ,niwaombe sana hasa wale wanaonunua vyuma chakavu ukinunua kibao cha ainahii utakuwa umeukaribisha umaskini,” alisema Mh Mayeka
“Niwaombe sana tuhimizane ,lakini zaidi tuvitunze na wote tuwe walinzi kwani faida ni ya kwetu sote, barabara hii ni miongoni mwa barabara ambazo leo tunaanza kuziwekea vibao vya utambulisho.”Aliongeza Mh Mayeka.
Muonekano wa Kibao cha Barabara ya Mapogoro kilicho wekwa na Mh Mayeka Simon Mayeka Mkuu wa Wilaya ya Chunya wakati wa Uzinduzi wa Barabara za Mitaa
Mkuu wa Wiaya ya Chunya Mh Mayeka Simon Mayeka watatu kutokea Kushoto Akiwa sambamba na DAS wa Wilaya ya Chunya Mh Michombero wapili kutoka Kushoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndg Tamimm Kambona mwenye Shati Jeupe na Afisa Aridhi wa Halmashauri ya wilaya ya chunya Sundy Mwakalebela wa kwanza kutoka kushoto wakiwa kwenye Uzinduzi wa Uwekaji wa Vibao vya Maelekezo kwenye barabara za Mitaa.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh Mayeka Simon Myeka Akiwa Ameshika kibao cha Mfanyo cha Namba ya Nyumba Wakati wa Uzinduzi wa uwekaji na Ubainishaji wa vibao vya Maelekezo vya Nyumba na barabara za Mitaa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.