Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S. Mayeka amewataka madereva bodaboda na madereva bajaji kubadirika ili kubadiri mitazamo hasi ya watu wengine dhidi yao akisema kwa kufanya hivyo watatoa mchango chanya kwa jamii yao na Taifa lao la Tanzania tofauti na ilivyo sasa
Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa juma wakati alipofanya mazungumzo na maafisa usafirishaji (Madereva bodaboda na madereva bajaji) wanaofanya shughuli zao ndani ya wilaya ya Chunya hasa maeneo ya Chunya Mjini kikao kilichofanyika ukumbi wa Mikutano Sapanja, huku akisema vikao hivyo vitakuwa na mwendelezo mpaka kuwafikia maafisa usafirishaji wote wanaofanya kazi zao ndani ya wilaya ya Chunya kwa ujumla wake.
“Wako watu wanabeza kazi yenu na kudharau kazi hii lakini mimi najua ninyi mumejenga, mnasomesha kupitia kazi hii na pia familia zenu zinawategemeeni sana badirikeni muanze sasa kuheshimu sheria za usalama barabarani kwa usalama wenu ninyi na usalama wa watumiaji wengine wa barabara”
Aidha Mkuu wa wilaya ya Chunya amewataka madereva Boda boda kuwa wazalendo kwa Chunya yao na Nchi yao kwa ujumla ili kuona uwezekana wa kusaidia taifa lao kupitia kazi yao kwa kufichua njama na siri nyingine ambazo zina manufaa makubwa kwa Chunya na Taifa kwani wao wanajua siri nyingi sana kupitia kazi yao ya usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka eneo moja kwenda eneo lingine.
“Madereva bajaji na madereva bodaboda mna siri nyingi sana kwanza kuhusu familia zetu na hata siri za watoroshaji wa madini na hata siri nyingine ambazo mkishirikiana nasi mtasaidia sio wilaya ya Chunya tu bali Taifa zima hivyo niwaombe kuwa wazalendo kwa nchi yenu ili tushirikiane kuhakikisha Chunya inasonga Mbele na hamiye Taifa kwa ujumla wake”.
Awali akitoa salamu kwa mkuu wa wilaya kwa niaba ya madereva bodaboda wenzake Mwenyekiti wa umoja wa waendesha bodaboda wilaya ya Chunya ndugu Samson Mwanswa alipeleka ombi lao la kupatiwa ofisi ili waweze kushiriki ipasavyo kusimamia taratibu na miongozo waliyojiwekea na hatimaye kutoa ushirikiano unaofaa kwa jeshi la polisi ukianzia kikosi cha usalama barabarani na baadaye jeshi la polisi kwa ujumla.
“Ombi letu ni moja tu kwako Mhe Mkuu wa wilaya, Tunaomba tupate ofisi na ombi hili tuliwahi kulileta katika ofisi yako na tuliambiwa kwakuwa ofisi nyingi zitahamia jengo jipya ambapo mpaka sasa ofisi zimeshahamia huko lakini ombi letu halijashughulikiwa hivyo tunaomba sana tupate ofisi ili kurahisha utendaji kazi wetu kwa ujumla wake”.
Kikao hicho cha Mkuu wa wilaya ya Chunya na maafisa usafirishaji yaani waendesha bajaji na waendesha bodaboda kimekuja ikiwa ni juhudi yake ya kuendelea kushirikisha wananchi katika kuleta maendeleo kupitia makundi mbalimbali kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha wilaya ya Chunya inakuwa salama wakati wote na wananchi wanafanya majuku yao ya kawaida kwa amani na utulivu
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka akizungumza na maafisa usafirishaji (Madereva boda boda na bajaji) katika ukumbi wa Mikutano Sapanjo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.