Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S.Mayeka amesema Banki ya NMB inaunga mkono Juhudu za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna wanavyotoa huduma zao kwa wananchi na kwa michango yao mbalimbali wanayoitoa kuhakikisha jamii inakuwa bora wakati wote
Kauli hiyo ameitoa leo 17/10/2023 kwenye viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Chunya wakati akipokea vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni tisa (9,000,000/=) vilivyotolewa na Banki ya NMB ili visaidie kupunguza changamoto kwenye sekta ya Afya na Elimu ikiwa ni sera ya banki hiyo kurudisha faida kwa wananchi ambao ndio wateja wa Banki hiyo.
“Nawashukuru sana banki ya NMB kwa huduma na mchango mkubwa ambao benki ya NMB inatoa kwaajili ya kusaidia jamii katika sekta ya afya na elimu Lakini pia kwa kwendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuhuri ya Muuungano wa Tanzania kwani mchango huo utasaidia kupunguza changamoto katika vituo vya afya vitakavyo nufaika na vifaa hivyo ambavyo ni kituo cha Afya cha Makongolosi pamoja na kituo cha Afya Kalangali pamoja na wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya Msingi Lupa”
Kaimu meneja wa kanda nyanda za juu wa banki ya National Bank of Commarce (NMB) ndugu Frank Rutakwa amesema kuwa suala la afya ni moja ya vipaumbele vyao kama Benki ili kuhakikisha afya za watanzania wanao wahudumia zinakuwa bora pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta ya afya
“Sisi kama Benki ya NMB afya ni kipaumbele chetu na ndio mana katika sekta ambazo tumejikita kusaidia serikali ni pamoja na sekta ya afya , lakini pia tunaunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katika sekta ya afya kama ambavyo Raisi wetu anaipa kipaumbele sekta ya afya’’alisema Rutakwa.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona ameishukuru benki ya NMB kwa mchango mkubwa ilioutoa ikiwa ni sehemu ya kile ambacho wanakipata na kuahidi kwamba wao kama Halmashauri wateendelea kutoa ushirikiano kwa Banki hiyo kama ambavyo wamekuwa wakishirikiana maeneo mbalimbali katika kulijenga Taifa.
Kwaniaba ya idara ya Afya wilaya ya Chunya, Mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya Daktari Elizabeth Nyema ameishukuru benki ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono sekta ya afya kwa kuwapatia vifaa mbalimbali ambavyo wamevitoa ili kuhakikisha wanaendelea kuwahudumia wananchi ipasavyo kwani afya ndio msingi wa uzalishaji mali si kwa mwananchi wa Chunya tu bali pia jamii ya watanzania wote.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na vitanda 10 vya kulazia wagonjwa, vitanda 2 vya kujifungulia wakinamama wajawazito pamoja na viti mwendo 7 kwaajili ya wanafunzi wenye ulemavu na vifaa hivyo vimepatikana ikiwa ni kutimiza lengo la Benki hiyo ya kurudisha fadhila kwa wateja wake ambapo kila mwaka shughuli mbalimbali za kijamii hufanyika.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S.Mayeka (Kulia na aliyevaa miwani) akimkabidhi kitanda cha kulazia wagonjwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona (Kushoto) baada ya kupokea vifaa hivyo kutoka kwa kaimu meneja wa Banki ya NMB nyanda za juu kusini
Kaimu meneja wa Benki ya NMB ndugu Frank Rutakwa (Mwenye suti ya blue), Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S. Mayeka (katikati aliyevaa miwani), Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu Kambona (anayetazama simu), anayefuata ni Mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya Daktari Elizabeth Nyema na anayemalizia upande wa kushoto ni Dr Darison Andrew mganga mkuu wa wilaya ya Chunya (Mwenye Shati la Blue)
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.