Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka amewashukuru na kupongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Wildlife Conservation Society (WCS) kwa kazi kubwa wanazozifanya katika kuisaidia serikali na jamii kwa ujumla wilayani Chunya.
Ametoa pongezi hizo leo 4/11/2023 kwenye kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kuhudhuriwa na Afisa uhifadhi wanyamapori wa Hamashauri ya wilaya ya Chunya, kamati ya usalama ya wilaya ya Chunya , kaimu katibu tawala na viongozi wengine wakiwepo viongozi mbalimbali wa shirika hilo kuanzia ngazi ya Taifa, Mkoa, Mratibu wa mradi na wafanyakazi wengine wa shirika hilo.
“Niwashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa ambazo mnazifanya Chunya kwa kufanya shughuli mbalimbali ambazo mnaisaidia serikali na mmeweka alama katika halmashauri ya Wilaya ya Chunya tunaona juhudi zenu na niseme tu kwakila kitu mnachohitaji milango iko wazi tunawakaribisha sana na tutawapatia ushirikiano wa kutosha” alisema Mhe. Mayeka
Aidha Mhe Mayeka amewaomba WCS wanapokutana na wafadhili wao kuendelea kuangalia namna ambavyo wataendelea kuwasaidia wananchi waliokubali maeneo yao kuhifadhiwa kwaajili ya mapitio ya Wanyama kwani katika maeneo hayo wananchi walikuwa wakiyategemea kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi kama kilimo , malisho mawindo pamoja na uvunaji wa asali kwaajili ya kujipatia kipato.
“Kama tunataka uendelevu wa mradi kwa maeneo hayo ya hifadhi ni vizuri kuiangalia jamii husika ya maeneo hayo na kuzisaidia juu ya shughuli ndogo ndogo ambazo wanaweza wakazifanya kwaajili ya kujipatia kipato ikiwa ni pamoja na kuwatengea maeneo ya malisho kwaajili ya mifungo yao kuwapandia nyasi kwaajili ya chakula cha mifugo lakini pia masoko kwaajili ya bidhaa zao kama vile asali. Aliongeza Mhe Mayeka
Awali akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi wa WCS Mkoa wa Mbeya Dr Luthando Dziba akiwawakilisha viongozi wa taasisi hiyo amemshukuru Mkuu wa wilaya kwa ushirikiano ambao wameendelea kuupata kwa kipindi chote kupitia mradi wa Kuhifadhi mapitio ya Wanyama yani Ruaha –katavi unaotekelezwa katika maeneo ya Sipa, Kambikatoto , Bitimanyanga na Mafyeko kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
‘’Tunashukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao tunaupata kutoka kwako na Viongozi wengine , tumekuwa na ushirikiano na mahusiano mazuri pia hata kwa jamii ambayo imetoa maeneo yao na tutakuwa na amani kama tutaacha alama kwa jamii ambako mradi huu unatekelezwa kwa kuangalia namna ambavyo na wao watanufaika’’ alisema Dziba
Shirika la WCS linatekeleza miradi yake katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania ambako wanatekeleza mradi wa kuhifadhi mapitio ya wanyama poli yani Ruaha –Katavi katika maeneo tofauti tofauti na Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ikiwa miongoni mwa maeneo hayo yanayonufaika na WCS.
Mkurugenzi wa WCS Mkoa wa Mbeya Dr Luthando Dziba akizungumza jambo wakati wa kikao cha shirika hilo na Mkuu wa wilaya ya Chunya kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chunya leo tarehe 4/11/2023
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka akizungumza kwa kushukuru mbele ya Uongozi wa WCS walipokuja ofisini kwake mapema leo tarehe 4/11/2023
Wajumbe wa kikao cha Mkuu wa wilaya ya Chunya na WCS Kilichoketi Mapema leo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.