Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo” wilaya ya Chunya ambapo jumla ya wahitimu 78 wamefuzu mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa miezi mine
Sherehe za kufunga mafunzo hayo zimefanyika leo Ijumaa Novemba 18, 2022 katika viwanja vya kijiji cha Lupatingatinga.
Akizungumza katika sherehe hizo, Mayeka amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia vyema mafunzo waliyoyapata huku akiwaasa kufanya shughuli za maendeleo ili kujiinua kiuchumi.
Mayeka amewataka wahitimu hao kuunda vikundi vya ujasiriamali ili serikali iweze kuwapatia mikopo ili iwasaidie kujikwamua kiuchumi.
Mikopo ipo na mkurugenzi analazimika kuitoa, kutoa mikopo ni lazima cha msingi waombaji wawe kwenye utaratibu na nyinyi tengenezeni utaratibu mzuri ili muweze kukopesheka.
Mayeka amesema kuwa anaimani mafunnzo hayo yamewajengea ukakamavu ujasiri na kujiamin kwani kwa sasa wahitimu watakuwa tofauti na ambavyo walikuwa hawajapatiwa mafunzo hayo.
“Hamja fundishwa mafunzo haya kwenda kuwatesa raia kuwaonyesha nyinyi mnajua kareti, hawa raia kaziyenu kubwa ni kuwalinda na kuwasaidia ili waweze kupate haki”
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya huyo amezitaka kampuni zote za ulinzi ndani ya wilaya ya chunya kutumia walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo
“Asiajiriwe mlinzi yeyote kama hajapitia mafunzo ya Mgambo, nimarufuku makampuni ya ulinzi kuwa na walinzi wasiokuwa na mafunzo ya mgambo”. Dc Mayeka alisisitiza
Aidha Mayeka amemtaka Mkuu wa polisi wilaya ya Chunya {OCD} kufuatilia na kuhakiki malindo yote ya binafsi na yasiyokuwa ya binafsi sambamba na makampuni yote ya ulizi, hairuhusiwi kuajiri mlinzi kama hajapitia mafunzo ya mgambo.
Wahitimu wa mafunzo ya Mgambo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Chunya
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mh. Mayeka S. Mayeka akikagua gwaride
Wahitimu wakitembea kwa Mwendo wa pole pole
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.