Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Chunya ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe Mayeka S Mayeka Mkuu wa wilaya ya Chunya Wameziagiza kamati zote za Ujenzi kuhakikisha vifaa vya ujenzi wa miradi ya BOOST vinanunuliwa kwa bei iliyoko dukani huku wakiwataka wajumbe wote wa kamati za ujenzi kuwepo eneo la mradi wakiwa na Nyaraka zote zinazohusu ujenzi huo ili kujibu hoja zinazotolewa na viongozi mbalimbali wanapokuja kukagua mradi husika
Mhe. Mayeka ametoa maelekezo hayo wakati alipoiongoza Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kwenye ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya Boost inayotekelezwa na Halmashauri, ziara hiyo imedumu kwa siku mbili kuanzia tarehe 31/5/2023 hadi tarehe 1/5/2023 ambapo miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 1.4 imetembelewa na kukaguliwa
Kamati hiyo imeshauri mambo mbalimbali ili utekelezaji wa miradi hiyo uwe wenye tija, Mambo hayo ni pamoja na;
Kwanza kuhakikisha kamati zote za ujenzi zinakuwepo eneo la mradi wakati wote ili kuhakikisha ufanisi wa utekelezaji wa mradi huo unakuwa wenye ubora
Pili, Kuhakikisha Nyaraka zote zinazohusiana na mradi huo zinapatikana katika eneo la mradi kila viongozi na kamati mabalimbali zinapotembelea miradi hiyo, Na nyaraka hizo ziwe zenye ukamilifu na zenye ukweli ili kuepuka usumbufu unaweza kujitokeza hapo baadaye
Tatu, Kamati imemwagiza mhandisi wa Halmashauri ya wilaya kuwepo eneo la mradi ili kuhakikisha ushauri wowote wa kitaalamu kwa mafundi wanaojenga mradi wanaupata kwa wakati ili kuepusha ucheleweshaji wa mradi huo
Nnne, Wamezielekeza kamati zote zinazosimamia mradi wa ujenzi wa Madarasa mawili katika Shule shikizi ya Mkange kwenda kuzungumza na Mzabuni anayewauzia vifaa vya ujenzi kupunguza bei ya saruji kutoka elfu kumi na nane (18000) na kuwa elfu kumi na saba na miatano (17500) kama ilivyo kwenye miradi mingine
“Kwanini mnunue saruji kwa bei kubwa kuliko miradi mingine yote wilayani Chunya? Kule Kanoge shule ya Msingi wananua saruji kutoka Chunya ambako ni mbali kuliko mnako nunua ninyi lakini wananunua kwa 17500/= ila ninyi 18000, hivyo tunawataka mzungumze na mzabuni wenu kupunguza bei hiyo” Alihoji Mwenyekiti wa kamati Mhe Mayeka
Vile vile kamati kupitia mwenyekiti wake imewataka wananchi kushiriki ipasavyo kwa namna mbalimbali ikiwa ni kusogeza fursa,zinazopatikana katika maeneo yao, kufika eneo la mradi na kuona maendeleo yake lakini kulinda mradi huo ili miradi hiyo ilete tija iliyokusudiwa maana lengo la miradi inayojengwa na serikali ni kuwasaidia wananchi.
Halmashauri ya wilaya ya Chunya ilipokea fedha kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni mia nne themanini na mbili na laki moja (1,482,100,000) kupitia mradi wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa shue za awali na Msingi (BOOST) ili kujenga shule mpya Mbili pamoja na kujenga madarasa mawili na ofisi moja kwa shule nane zilizoteuliwa. Shule Mpya moja inajengwa kata ya Makongolosi na Nyingine inajenwa kata ya Mafyeko ambapo kila moja imetengewa milioni mia tano thelasini na nane na laki tano (538.500.000/=)
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.