• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

Imewekwa: April 4th, 2025

Waziri wa madini Mhe. Antony Mavunde amelipokea ombi la Wakuu wa Wilaya kutoka katika Wilaya ya Chunya na Wilaya ya Songwe juu ya kuongeza kufanya utafiti wa madini katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hizo ili kuongeza uzalishaji wenye tija katika sekta hiyo na hatimae kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kukuza pato la Taifa kwa ujumla

Ombi hilo limetolewa na Wakuu wa Wilaya kwa Waziri wa Madini tarehe 03/04/2025 wakati wa hafla ya uzinduzi wa shughuli za uchimbaji wa madini  wa Porcupine North unaofanywa na kampuni ya Shanta Gold mining Company LTD .

“Ombi la Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaj Batenga na Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Solomon Itunda nimelisikia juu ya kuongeza utafiti wa madini katika meneo mbalimbali ili kuongeza tija ya serikali katika kupata mapato kupitia sekta hii ya madini, Waheshimiwa wakuu wa Wilaya nakubaliana nanyi hatuwezi kuiendeleza sekta ya madini pasipo kufanya utafiti wa kina kwasababu utafiti ndio moyo wa ukuwaji wa   sekta ya madini” alisema Mhe. Mavunde

Aidha Mhe. Mavunde ameongeza kuwa Mhe Rais aliwaongezea bajeti sekta ya madini na  kiasi kikubwa cha bajeti  hiyo kimeelekezwa katika kufanya utafiti wa kina  kwa lengo la kukuza sekta kwani imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa katika  kuongeza pesa za kigeni na kukuza  pato la Taifa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbaraka Alhaji Batenga mbali na kutoa ombi la kuongeza utafuti wa madini katika maeneo mbalimbali pia ameishukuru kampuni ya Shanta Gold Mining kwa kuanza Shughuli za uchimbaji kwani kupitia kampuni hiyo wazawa watajipatia ajira lakini pia  wachimbaji wengine watapata ujuzi kupitia  kampuni hiyo  na serikali kujiongezea mapato  na hatimaye kukuza uchumiwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

  Awali akitoa salam za Chama Mwenye kiti wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Noel Chiwanga ametoa rai kwa mwakezaji kutumia fursa kwa tija kubwa lakini pia kuhakikisha wazawa wanakuwa kipaumbele katika kufanya kazi mbalimbali katika kampuni hiyo ili na wao waweze kunufaika na uwekezaji huo

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Shanta Ndugu Honest Mrema Akisoma taarifa kwa Mgeni rasimi amesema kuwa lengo la kampuni ni kuendelea kufanya utafiti wa kina kwenye maeneo yote ya leseni ili kuongeza maisha ya mgodi kwa miaka mingi ijayo na kwa mwaka huu wa 2025 Kampuni imetenga  zaidi ya billioni 12 kwaajili ya utafiti wa madini kwenye eneo la Lupa ili kukuza shughuli za uzalishaji wa madini Nchini.

Akiongea kwa niaba ya wachimbaji wadogo Ndugu Abraham Mwakyalagwe Ameishukuru serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kukuza sekta ya madini na kuwapigania wachimbaji wadogo  huku akitoa ombi juu ya uboreshwaji wa miundo mbinu ya barabara pamoja na ujenzi wa Soko  kubwa la kisasa  katika Wilaya ya Songwe.

Uzinduzi wa shughuli za uchimbaji wa Madini katika mradi wa Porcupine North umehudhuriwa na  , waziri wa madini , Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya  kutoka Mbeya na Songwe Kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya na Mkoa , wafanyakazi wa Shanta Gold Mining , Viongozi wa mila na  Wananchi  wanao zunguka aneo la mgodi ,

Waziri wa madini Mhe. Antony Mavunde akizungumza na hadhira wakati wa hafla ya uzinguzi wa shighuli za uchimbaji madini wa porcupine North unaofanywa na kampuni ya Shanta Gold Minging  Wilayani Chunya.

Viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Mbeya na Songwe wakishuhudia Waziri wa madini akikata utepe kuashiria rasmi kuanza kwa shughuli za Uchimbaji wa madini mradi wa porcupine North .

Mkuu wa Wilaya ya Chunya upande wa  kushoto na Mkuu wa Wilaya ya Songwe upande wa kulia wakiwa wameambatana na Waziri wa madini Mhe Antony Mavunde  alievaa kofia pamoja na Mkurugenzi  Mwendeshaji wa kampuni ya Shanta Gold Mining.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Shanta Gold Mining baada ya hafla ya uzinduzi wa shughuli za uchimbaji mradi wa Porcupine North  

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • TARAFA YA KIPEMBAWE CHUNYA YAJIDHATITI KUWATUMIKIA WANANCHI.

    March 21, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.