Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya kila mmoja kushiriki katika kutunza, kulinda na kuendeleza vyanzo vya maji vilivyopo wilayani humo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo
Ametoa kauli hiyo leo 8/9/2023 wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhudia mitambo ya kuchimba visima ikiendelea na zoezi la uchimbaji wa kisima cha maji katika kata ya Upendo ikiwa ni mwendelezo wa azma ya serikali kuchimba visima 26 vya maji katika halmashauri ya wilaya ya Chunya na kata ya Upendo ni miongopni mwaka kata zitakazonufaika na mradi huo
“Kila mwananchi awe mlinzi wa mwenziye si kwa kipindi hiki cha maandalizi ya mbio za Mwenge wa uhuru tu bali kwa kipindi chote, Lakini pia wako watu watafungwa msishangae maana sheria zipo zinazokataza watu kuharibu mazingira hivyo lindeni maeneo ya vyanzo vya maji ili maji yaendelee kuwepo hata kwaajili ya vizazi vijavyo”
Aidha Mhe. Mayeka amewataka wananchi wa kata ya Upendo kuhakikisha eneo hilo halitumiki kama sehemu ya malisho au sehemu ya kufyatua tofali kwani kufanya hivyo mtakuwa mtakuwa mnaharibu chanzo hiki cha maji jambo linaloweza kupelekea maji kupungua na hatimaye kukosekana kabisa hivyo tunzeni kisima hiki vizuri
“Tafadhali sana linden kwa pamoja kisima hiki na eneo lote la chanzo cha Maji na kwa kufanya hivyo mtakuwa mmemuunga mkona Mama yetu Mpendwa Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani ndiye aliyenunua mitambo hii mnayoiona ili wanachunya na watanzania kwa ujumla wapate maji”
Naye Diwani wa kata ya Upendo Mhe.Richard N. Itelekelo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Upendo ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwanza kupata mitambo ya maji lakini pia Kata ya Upendo kuwa miongozi mwa wanufaika wa moja kwa moja wa mitambo hiyo ya Uchimbaji wa maji na ameahidi kuendelea kulinda kisima hicho pamoja na vyanzo vya maji vilivyopo katika kata ya Upendo
Mradi wa Uchimbaji wa visma wilayani Chunya unataraji kuchimba visima 26 na utagharimu fedha kiasi cha shilingi milioni mia tisa na kumi (910) mpaka kukamilika kwake na kisima hicho kinachochimbwa kata ya upendo kitawakilisha visima vingingine vyote vinavyochimbwa wilayani Chunya kwa kupitiwa na mwenge wa uhuru mwaka 2023 ambapo kwa wilaya ya Chunya utakimbizwa tarehe 13/09/2023.
Diwani wa kata ya Upendo Mh. Richard N. Itelekelo akitoa salamu za wananchi wa kata ya Upendo kwa Mkuu wa wilaya ya Chunya alipotembelea kuona namna kazi inavyoendelea katika kata hiyo
Baadhi ya wananchi wa kata ya Upendo waliojitokeza kushuhudia utekelezaji wa ahadi za serikali ya awamu ya sita katika sekta ya maji kwa wananchi muda huo wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chunya alipotembelea kuona maendeleo ya kazi ya kuchimba kisima katika kata ya Upendo
Mtambo wa kuchimba visima vya maji chini ya wahandisi wa maji ukiendelea na kazi ya kuchimba kisima katika kata ya upendo, Mbele ya picha hiyo kunaonekana baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia namna zoezi la kuchimba maji likiendelea
Wahandisi wa maji wakiendelea na kazi ya kuchimba kisima cha cha Maji katika kata ya Upendo na Pembeni kidogo wananchi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya alipotembelea kuona zoezi la uchimbaji wa maji linavyoendelea katika kata ya Upendo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.