Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga amewataka viongozi wa vijiji na kata kuhakikisha wanaweka vizuri Nyaraka za kumbukumbu za umiliki wa maeneo ambapo miradi mbalimbali ya Maendeleo inajengwa ili kuepuka migogoro ya ardhi mbele pindi kizazi hiki kitakapokuwa kimepita
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 28/05/2024 wakati akiongoza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Chunya wakiambata na wataalamu kutoka taasisi mbalimbali za Serikali katika wilaya ya Chunya ili kukagua utekelezaji wa mradi wa maji unaojengwa na shirika la Catholic Relief Services (CRS) kwa gharama ya shilingi milioni mia tatu hamsini na tano
Akitoa Taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama, Meneja wa mradi huo kutoka Shirika na CRS Bi Bertha Mkepela amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia themanini huku akisema mwishoni mwa mwezi juni mradi huo utakuwa umekamilika
Diwani wa kata ya Kasanga Mhe Mh. Benson B. Msomba amewashukuru wadau kutoka shirika la CRS kwa namna ambavyo wanatekeleza ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya Kasanga kwani kupitia mradi huo utapunguza uhitaji wa Maji kwenye kata ya Kasanga maana Kijiji cha Soweto kikipata maji maana yake uhitaji wa maji utabaki kwenye kijiji cha Mawelo
“Shukrani kubwa ni kwa Ziara yako wewe Mkuu wa wilaya ya Chunya na Uongozi ulio ongozana nao pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweza kutubarikia mradi huu katika kijiji cha Soweto. Mradi huu utapunguza changamoto ya maji kwenye kijiji cha Soweto na najua baada ya kutatua hili kijiji cha Mawelo kitafuata. Mhe Mkuu wa wilaya tupelekee salamu zetu kwa Mhe Rais kwamba Wananchi wa Kata ya Kasanga wanakushukuru sana kumtua Mama Ndoo Kichwani”. Amesema Mhe Msomba
Kamati ya Ulinzi na usalama wakiambatana na viongozi kutoka Taasisi Mbalimbali wameanza rasmi ziara ya siku tatu kukagua miradi ya maji inayotekelezwa wilayani Chunya. Ziara hii kwa siku ya kwanza imehusisha kata ya Matundasi, Kata ya Kasanga na kata ya Chalangwa na ziara hiyo itaendelea tena kesho tarehe 29/05/2024 kuendelea kukagua utekelezaji wa Miradi ya maji wilayani Chunya
Diani wa kata ya Kasanga Mhe Benson Msomba akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Usalama ya wilaya ya Chunya ilipotembelea mradi wa maji unaotekelezwa na CRS kwenye kijiji cha Soweto kata ya Kasanga
Meneja wa RUWASA wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Aliyevaa shati Nyeupe na ameshika karatasi Mkononi) akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Batenga (Aliyavaa shati la drafti) wakati alipoongozana na kamati ya usalama ya wilaya kukagua mradi wa Maji Soweto
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Batenga (Aliyevaa shati la Drafti) akiwa sambamba na Mhe Diwani wa kata ya Kasanga Mhe Msomba mapema leo wakitembea kutoka eneo la mradi wa kisima cha Maji kilichochimbwa na CRS kwa lengo la kutatua Changamoto ya Maji katika kijiji cha Soweto kata ya Kasanga
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.