Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Alhaj Mbaraka batenga amesema kuwa anaimani na wadau katika kuchangia shughuli mbalimbali za Maendeleo katika halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwani wamekuwa wa kijitoa sana kwa hali na mali katika Sekta mbalimbali ikiwemo Michezo ambapo wadau hao walianza kushiriki tangu ujenzi wa Uwanja wa Michezo ulipoanza mwaka 2013
Kauli hiyo ameitoa tarehe 24/05/2024 wakati wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Uwanja wa Mpira Wilaya ya Chunya iliyofanyika katika Ukumbi wa Omary City uliopo kata ya Itewe
“Mimi nina Imani sana na wadau hawa hawajawahi kutuangusha katika shughuli mbalimbali za Maendeleo katika Wilaya yetu , tunatamani ifikapo mwezi wa nane Uwanja uwe umekamilika ili timu ziweze kuja kucheza chunya kwani tunataka kuileta Tanzania Chunya na Chunya tuipeleke Tanzania.alisema “Mhe. Batenga
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera mgeni rasmi wa Hafla hiyo amesemakuwa kunafaida nyingi timu zinapokuja kushiriki ligi katika viwanja vya Chunya kwani Wafanyabiashara mbalimbali wa hotel , Mamalishe na wasafirishaji itakuwa ni fursa kwao kufanya biashara na kujipatia kipato kwaajili ya kukuza uchumi wao pamoja na Halmashauri kujipatia mapato na hatimaye kukuza uchumi wa Chunya
“Uwepo wa timu kushiriki ligi kuu hapa watu wenye magari mtafanya biashara sana, watu wenye Hotel watu watalala hapa, Hotel zote zitajaaa lakini pia mama lishe nao watafanya biashara kwani kunapokuwa na mechi watu wengi sana wanasafiri na timu jambo ambalo litapelekea kukuza uchumi wa Chunya na Halmashauri itajipatia mapato Chunya”alisema Mhe.Homera
Aidha Mhe Homera ameongeza kuwa Timu mbalimbali zinapokuja kucheza ligi katika uwanja wa Chunya itakuwa ni moja ya fursa ya kukuza uwekezaji pamoja na kukuza utalii kutokana na ujio wa watu kutoka seheme tofauti tofauti hali ambayo itapelekea Wilaya ya Chunya kuendelea kufanya vizuri katika kutekeleza ilani ya Chama cha mapinduzi kwa asilimia mia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Michezo.
Akitoa Salama katika harambee ya kuchangia Ujenzi wa Uwanja wa Michezo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ndugu Noel Chiwanga ametoa rai kwa wadau kwendelea kuwa wazalendo kwa kumuunga Mkono Mkurugenzi wa Timu ya Kengold ndugu Keneth Mwakyusa ili kwendeleza Michezo katika Wilaya ya Chunya kwani kwa kufanya hivyo italeta hamasa kwa wadau wengine kuunga Mkono sekta ya Michezo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Athumani Bamba amewashukuru Wadau kwa kwendelea kushirikiana na halmashauri katika shughuli mbalimbali za maendelao katika shughuli mbalimbali za Maendeleo na kuwaomba kuunga mkono jambo la Ujenzi wa Uwanja wa Michezo ili uwanja uweze kukamilika na kutumika kwaajili ya michezo mbalimbali.
Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Uwanja wa Michezo Wilaya ya Chunya imeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera ambapo michanho mbalimbali imeweza kutolewa na wadau ikiwa ni pamoja na Mifuko ya Saruji 400, Mchanga roli 10, fedha taslimu Milioni 3,240,000/= ahadi milioni 61,669,000/= pamoja na Kokoto zenye thamani ya shilingi milioni kumi (10,000,000/=) lengo ikiwa ni ukamilishaji wa Uwanja wa Michezo unaomilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Zuberi Homera akizungumza na Wadau wa Soka pamoja na Wadau wa Maendeleo wakati wa Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Uwanja wa Michezo Wilaya ya Chunya iliyofanyika katika Ukumbi wa Omary City uliopo kata ya Itewe.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ndugu Noel Chiwanga akitoa Salam za Chama wakati wa harambee ya kuchangia Ujenzi wa Uwanja wa Michezo Wilaya ya Chunya iliyofanyika katika Ukumbi wa Omary City .
Kaim Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Athumani Bamba akiwashukuru Wadau wa Maendeleo kwa kwendelea kujitoa kwa hali na mali katika shughuli mbalimbali za Maendeleo hayo ameyasema wakati wa harambee ya kuchangia Ujenzi wa Uwanja wa Michezo.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.