Mkuu wa wilaya ya Chunya Mrakibu mwandamizi wa Uhamiaji Mhe.Mbaraka Alhaji Batenga amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya kusitisha mara moja biashara ya Mkaa kwani inachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira na kusababisha ukame hivyo ametaka kuacha biashara hiyo kwa maslahi ya kizazi cha sasa na chakizazi cha badaye.
Kauli hiyo ameitoa leo Desemba 23/2023 alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua eneo alilopewa mwekezaji Long pin Tanzania lililopo kata ya Nkung’ungu eneo ambalo mwekezaji anaetaka kuendesha shughuli za kilimo cha zao la Soya.
“Nataka biashara ya uvunaji wa mkaa ife mimi sipendi biashara ya mkaa kwasababu inaharibu mazingira, hii mvua mnayoiona inanyesha ni kwasababu ya hii miti manayoiona kwahiyo anzeni kujipanga kwa biashara nyingine na si biashara ya mkaa” alisema Mhe. Batenga.
Aidha amewataka kuhakikisha wanazuia ukataji wa miti hovyo na kutaka kukamatwa na kuchukuliwa hatua watu wote watakaojihusisha na ukataji wa miti bila kibali huku akiwashauri wananchi wa wilaya ya Chunya kuangalia shughuli nyingine za kufanya ambazo ni rafiki kwa mazingira ikiwa ni pamoja na kuvuna asali badala ya kukata miti kwaajili ya kuchoma mkaa.
Awali akitoa salamu katibu Tawala Wilaya ya Chunya Ndugu Anakleth Michombero amewapongeza viongozi wa Nkung’ungu kwa kusimamia vizuri fedha zinazoletwa tutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya kata hiyo
Naye afisa kilimo Wilaya ya Chunya ndugu Cuthbert Mwinuka amesema kuwa kupitia uwekezaji wa Long pin Tanzania wananchi wa Nkung’ungu watanufaika na uwekezaji huo ikiwa ni pamoja na kujifunza kilimo cha Soya kibiashara, miundo mbinu ya umeme na barabara ya kutoka Lupa mbaka Nkung’ungu
Akitoa kero kwa Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya wana kijiji wenzake wa Nkung’ungu ndugu Menison Yohana mwananchi wa kijiji cha Nkung’ungu amesema kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili ni pamoja na migogoro ya mipaka kati ya kijiji cha Nkung’ungu na kijiji cha Ngwala ambapo wameomba kero hiyo iweze kutafutiwa ufumbuzi mapema.
Katika ziara yake Mhe. Batenga ametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa nguvu za wananchi katika kijiji cha Nkung’ungu ikiwa ni pamoja na jengo la ofisi ya kijiji, Nyumba za walimu, ujenzi wa vyoo vya wanafunzi,Pamoja na Mradi wa ujenzi wa shule ya wasichana inayojulikana kama Mayeka sekondari iliyyopo kata ya Lupa.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga akitoa maelekezo kwa viongozi alioambatana nao wakati wa kukagua eneo alilopewa muwekezaji ili kuanza kilimo cha Soya
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Batenga akikagua ujenzi unaoendelea wa miundombinu ya Shule ya sekondari ya wasichana Mayeka inayojengwa katika kata ya Lupa
Muonekano wa Shule ya sekondari ya wasichana Mayeka inayojengwa kata ya Lupa tayari kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2024
Baadhi ya wananchi na viongozi waliojitokeza kumsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Batenga aliptembelea kijiji cha Nkung'ungu mapema leo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.