Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mhe. Mubarak Alhaji Batenga amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Tamim Kambona kuhakikisha Klabu zote zilizopo Mashuleni zinakuwa na walimu walezi pamoja na kuhakikisha wanajengewa uwezo ili waweze kuzisimamia vyema klabu hizo ili klabu zitekeleze lengo lake ipasavyo.
Maagizo hayo ameyatoa Februari 24/2023 Wakati wa Maadhimisho ya siku ya mwazilishi wa Skauti duniani ambapo Halmashauri ya wilaya ya Chunya yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kipoka kata ya Bwawani na Mkuu wa wilaya ya Chunya alikuwa Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo
“Natoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha kwamba haya maeneo yote yani klabu ya Skauti , klabu ya kupinga rushwa, klabu ya mali hai ,klabu ya lishe na Ukimwi klabu zote hizi zipate walimu walezi na ziwe na wanachama kuanzia Shule za Msingi hadi Sekondari kwasababu huko ndiko tunakoaanza kuwaandaa na kuwajenga hawa vijana kuwa wazalendo kwaa Taifa lao “alisema Mhe.Batenga
Aidha Batenga aliongeza kuwa ni vizuri wanafunzi kujitafutia sifa za ziada wanapokuwa shule kwa kujiunga na klabu mbalimbali ambazo zitawawezesha kujifunza mambo mengi yenye manufaa kwao na taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuwajenga kuwa wazalendo na taifa lao ,watunzaji wa mazingira , wapinga rushwa pamoja na mambo mengine lakini pia klabu zitawasaidia katika maisha yao ya baadae kwenye soko la ajira.
“Sifa za ziada na misingi ya uzalendo itajengwa kupitia Skauti , kilabu za kupinga rusha , Lishe ,Ukimwi na klabu za mali hai tunasema hawa ni wazalendo kupitia matendo kwani uzalendo ni vitendo tukakupima uzalendo kupitia viashiria vya uzalendo ambavyo tunaviangalia huku huku kwanye klabu zetu “alisema Mhe. Batenga
Wakiongea kwanyakati tofauti Afisa elimu Msingi mwalim John Gwimile na Afisa elimu Sekondari mwalim Hamis Mapoto wamewapongeza Skauti kwa kazi nzuri wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya Shule na kuwataka waitunze miti hiyo vizuri kwa kuhakikisha wanaimwagilia maji wakati wa kiangazi ili miti hiyo iweze kustawi vizuri .
Akisoma risala kwa Mgeni rasmi kamishina wa Skauti Wilaya ya Chunya ndugu Joseph Kansato amesema kuwa katika klabu yao ya skauti wao kama wanachama wamekuwa wakifanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa mafunzo kwa vijana katika makambi,kufanya usafi katika maeneo ya jamii, upandaji wa miti pamoja na kushiriki matukio mbalimbali ya kitaifa kama vile Kukimbiza Mwenge na matukio mengine .
Kwa niaba ya wanachama wengine wa Skauti Crispa Obeth kutoka Kipoka sekondari kidato cha (II)na Gradness Mwakyembe darasa la (V) kutoka Shule ya Msingi Bwawani wamesema kupitia Skauti wamejifunza mazoezi ya kujenga afya zao lakini pia wamejifunza kuwa wazalendo kwa Taifa lao jambo hilo huwasaidia kujua histoia ya Taifa lao na uzalengo wa viongozi waliotangulia
Maadhimisho ya mwazilishi wa Skauti duniani huazimishwa kila mwaka ifikapo 22 Februari ambapo kitaifa kilele cha maadhimisho hayo kimefanyika tarehe 24 Februari 2024 ambapo Wilayani Chunya wameadhimishwa kwa kupanda miti 300 katika maeneo ya Shule ya Sekondari Kipoka na kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Skauti mmoja mti mmoja”
Mkuu wa Wilaya ya Chunya mhe.Alhaji Batenga katikati akiwa ameambatana na Kaim Kamishina wa Skauti aliesimama upade wa kulia ndugi Ambakisye Mwambije wakielekea viwanja vya Shule ya Sekondari Kipoka
pamoja na wanachama waskauiti
Mhe.Batenga akizungumza na wanachama wa Skauti pamoja na maafisa mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya mwazilishi wa Skauti yalitoazimishwa ki Wilaya katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kipoka.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.