Mkuu wa Wilaya ya Chyunya Mhe.Mbaraka Alhaji Batenga amewataka Maafisa Maendeleo ya jamii kuwa walezi wa vikundi vilivyokopeshwa na Halmashauri katika maeneo yao ili kuweza kuvifuatilia kwa karibu kujua vinafanya nini na kufanya tathimini kila robo ili kuona mwenendo mzima wa mkopo huo unaendaje , na kama kunachangamoto yoyote itakayopelekea kikundi kushindwa kurejesha mkopo huo kuweza kuitatua changamoto hiyo mapema .
Kauli hiyo ameitoa Mhe.Batenga leo Tarehe 31/1/2025 wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi ya Shilingi Millioni 803, 200,000 kwa Vikundi 83 vya Wanawake Vijana na Watu wenye ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ( Sapanjo)
“ Maafisa maendeleo ya jamii wote kwenye maeneo ambayo vikundi hivi vimechukua mkopo ninyi mkawe walezi wa vikundi hivi , lazima muwe na ratiba ya mwaka mzima ya kupitia vikundi hivi na kuvifanyia tathimini ili kama kunakikundi kinataka kwenda vibaya kisaidiwe mapema kabla mambo hayajaharibika natujue tunafanya nini, kwahiyo nawakabidhi ninyi kwa maafisa Maendeleo ya jamii wakawe walezi wenu.” alisema Mhe. Batenga
Aidha Mhe. Batenga ametoa msisitizo kwa vikundi vyote vilivyokopeshwa kuhakikisha vinarejesha Mkopo huo kwa wakati ili kuviwezesha ni vikundi vingine kunufaika na mkopo huo wa asilimia 10% unaotolewa na Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kwani ni mkopo usio kuwa na riba yoyote ,kikundi kinarejesha tu kiasi cha Mkopo uliokoposhwa.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde ametoa rai kwa vikundi kutokukopa kwa kufuata mkumbo bali wakope fedha hizo kwaajili ya kufanyia shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara pamoja na shughuli zingine za kuwaongezea kipato ili waweze kurejesha mkopo huo pamoja na kunufaika wao kama kikundi na mtu mmoja mmoja na hatimae Taifa kwa ujumla.
Afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Chunya Bi Marietha Mlozi akisoma taarifa kwa mgeni rasmi amesema kuwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kabla ya kupewa mikopo hiyo wamewajengewa uwezo juu ya usimamizi wa vikundi, usimamizi na uendeshaji wa miradi , utunzaji wa kumbukumbu , kuweka akiba na mambo mengine mengi yatakayo saidia vikundi hivyo viweze kujiendesha kwa ufanisi.
Goodanswer Richard kutoka kundi la vijana wengine na Ernest Itelekelo kutoka kundi la watu wenye ulemavu wakiwakilisha vikundi vilivyopata mkopo wameishukuru serikali ya Dkt samia suluhu Hassan kwa kurudisha tena mkopo wa asilimia 10% unaotolewa na halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kwani mkopo huo hauna riba tofauti na mikopo inayotolewa na taasisi zingine , Lakini pia wamewasihi wenzao waliopata mkopo huo kurejesha kwa uaminifu ili waweze kuaminika na kukopeshwa tena wakati mwingine.
Hundi ya shilingi Millioni 803,200,000 imetolewa kwa vikundi vya wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu ikiwa ni asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo vikundi vya wanawake ni 41, vikundi vya vijana 38 na vikundi vya watu wenye ulemavu 4 kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili ya kuomba mikopo yenye thamani ta shilingi million 1,260180.53 itaanza tarehe 10/12/2025.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akiwafunda wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi millioni 803,200,000.
Mmwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe Bosco Mwanginde akiwasihi vikundi vya wanawake , vijana na watu wenye ulemavu kuwa waaminifu katika kurejesha mkopo waliopewa na Halmashauri wa asilimia 10.
Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii Wilaya ya Chunya Bi Marietha Mlozi akisoma taarifa kwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi millioni 803,200,000 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akiwakabidhi hundi ya shilingi millioni 803,200,000 vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kataika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri (Sapanjo).
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.