Mkuu wa Wilaya ya Chunya amewataka wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba Wilaya ya Chunya kutenda haki na kudumisha nidhamu wakati wote ikiwa ni pamoja na utii nakufuata maelekezo yanayotolewa na viongozi na jamii kwa ujumla ikiwa ni moja ya vigezo vya kuwa askari bora wa jeshi la akiba kwa kufanya hivyo itawasaidia kupata kipaumbele kwenye fursa mbalimbali za ajira zitanapotolewa
Kauli hiyo ameizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo ya kijeshi kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Matundasi, tarafa ya Kiwanja jana Tarehe 20 Novemba 2024
“Leo hapa kwenye risala imesema mumehitimu mafunzo askari 106 kati ya 240 muliojiandikisha wengine wameshindwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, niwatake ninyi muliohitimu leo kutenda haki na kudumisha nidhamu muliojifunza wakati wa mafunzo ” alisema Mh. Batenga.
Mhe. Batenga amemtaka Diwani wa Matundasi Mh. Kimo John Choga pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama Wilaya ya Chunya kuwatumia askari wa jeshi la akiba waliohitimu mafunzo yao kwenye kazi mbalimbali za ulinzi na usalama kwenye kata, tarafa na Wilaya ili kuendelea usalama wa raia na mali zao huku akiwata sungusungu waingizwe kwenye mafunzo yajayo ya jeshi la akiba ili wafanya kazi kwa weledi “Mahala ambapo jeshi letu halipo, jeshi hili la akiba litumike kufanya kazi, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama muliopo hapa muwatumie jeshi hili kwenye shughuli mbalimbali za ulinzi na usalama za Wilaya lakini pia askari sungusungu waingizwe kwenye mafunzo yajayo ya jeshi la akiba ili wafanye kazi kwa weledi zaidi
Akisoma risala kwa mgeni rasmi mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba, ndugu Benedicto Obino amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Batenga kuwapa kipaumbele wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba kwenye fursa mbalimbali za ajira kama Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), ulinzi na usalama kwenye taasisi za serikali na sizizo za kiserikali.
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya tunaomba kupewa kipaumbele kwenye fursa za ajira kama Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ulinzi na usalama kwenye taasisi za serikali kama vile ofisi za Mkuu wa Wilaya, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Hospitali na taasisi zingine sizizo za kiserikali” amesema Obino.
Vilevile, Obino aliongeza kuwa, changamoto walizokutana nazo wakati wa mafunzo ni pamoja na mitazamo hasi kwa jamii na kubeza kuwa mafunzo hayo ni kwaaliokosa kazi, utoro, maradhi na ajali ambapo zimepelekea kati ya askari 240 waliojiandikisha waliohitimu mafunzo ni askari 106.
Naye Diwani wa Kata ya Matundasi, Mhe. Kimo John Choga amewashukuru wadau mbalimbali kwa kuchangia mahitaji muhimu kwa wakufunzi wa mafunzo ya jeshi la akiba pamoja na kumpongeza Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya, Anakleth Michombero kwa usimamizi mzuri wa mafunzo hayo mpaka kufanikisha wahitimu 106 kufuzu mafunzo hayo ya jeshi la akiba.
Mafunzo hayo ya jeshi la akiba yamehitimishwa tarehe 20 Novemba 2024 yamedumu kwa muda wa miezi minne tangu yalipoanza Julai 1, 2024 ambapo jumla ya askari 106 wamafanikiwa kuhitimu mafunzo hayo , wanaume wakiwa 89 na wanawake 17.
Wanafunzi waliohitimu mafunzo ya jeshi la akiba wakionesha umahiri wao wa utimamu wa mwili mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, jana wakati wa kuhitimisha mafunzo kwenye viwanja vya shule ya msingi Matundasi iliyopo Kata ya Kiwanja Wilaya ya Chunya, mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh. Mbaraka Alhaj Batenga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba na kamati ya ulinzi na Usalama na viongozi wengine wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi la akiba yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya shule ya msingi Matundasi, Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.