Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Alhaj Batenga ametoa siku kumi kwa mkandarasi na kamati ya ujenzi wa shule Sekondari Nkung’ungu kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na miundombinu ya shule hiyo ili wanafunzi wa kidato cha kwanza waliochaguliwa kujiunga na shule waanze masomo.
Mhe. Batenga ameyasema hayo Januari 14, 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika tarafa ya Kipembawe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“ Natoa siku kumi, na sitoongeza hata siku moja kwa mkandarasi na kamati ya ujenzi kukamilisha ujenzi wa shule ya sekondari Nkung’ungu, nataka muongeze muda wa kufanya kazi ili wanafunzi waanze masomo” amesema Mhe. Batenga.
Aidha, Mhe. Batenga amemtaka mzabuni wa mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Nkung’ungu kurudisha fedha za usafirishaji wa vifaa vya ujenzi kwakuwa mkataba waliongia shule na mzabuni huyo ulikuwa na kipengele cha usafirishaji na ufikishaji wa vifaa vya ujenzi kwenye eneo la ujenzi lakini mzabuni ametoa tu vifaa pasipo hakuvifikisha eneo la ujenzi.
“Namtaka mzabuni wa mradi, arudishe fedha za ufikishaji vifaa vya ujenzi, mkataba ulisomeka kuwa ata fanya ‘supply and delivery’ lakini kazi ya kufikisha vifaa imefanywa na Halmashauri ikishirikiana na kamati ya Ujenzi” amesisitiza Mhe. Batenga.
Vile Vile Mhe. Batenga amemtaka mhandisi wa mradi wa ujenzi kuhakikisha ubora na viwango vinazingatiwa katika ujenzi kama inavyoelekezwa kwenye mchoro wa usanifu wa ujenzi wa shule hiyo kwakuwa serikali imepelekea pesa ya ujenzi kulingana na gharama zilizooneshwa kwenye mchoro wa ramani.
Naye Mwenyekiti wa Kamati wa Ujenzi wa shule ya Sekondari Nkung’ungu, Mwalimu Erasto Kilasi amemuahidi Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Batenga kuwasimamia kikamilifu wasambazaji wa vifaa vya ujenzi na mafundi ujenzi kuharakisha ujenzi wa shule kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha ili shule hiyo ikamilike kwa muda uliopangwa.
Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari Nkung’ungu iliambatana na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya , Kamati ya Ulinzi na Usalama imekagua mradi wenye thamani ya Ths 583,180,028 ambazo ni fedha kutoka serikali kuu.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.