KATIBU Tawala wa wilaya ya Chunya, Anaklet Michombero amewataka maafisa elimu pamoja na walimu wote kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa miongozo ya usimamizi na uboreshaji wa elimu Msingi na Sekondari iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri, Michombero aliwataka maafisa elimu wilaya kuhakikisha wanakuwa wabunifu na kufanya vitu ambavyo vitaongeza ufaulu katika shule zao.
“Kama watumishi wa idara hii nyeti ya elimu, tunapaswa kuwa wabunifu na akili zetu ziwaze haraka na kwa ufanisi zaidi vitu vipya ambavyo vipo nje ya vile tulivyosomea. Kila mmoja wetu hana budi kujiongeza na kubuni namna mpya ya kuongeza ufanisi na ufaulu,”
“Wakuu wa shule na maafisa elimu tukajitahidi sana tuwe wabunifu tufanye vitu ambavyo wakati mwingine havipo kwenye miongozo yetu ila ilete tija kwenye elimu,” alisema Michombero.
Awali katika hafla hiyo, Afisa Elimu Awali na Msingi wa wilaya, Fred Mhanze alibainisha miongozo mitatu ambayo imezinduliwa kuwa ni mwongozo wa kwanza ni ule ambao umeainisha changamoto katika elimu ya msingi na sekondari.
Mhanze aliutaja mwongozo wa pili ambao unahusu mkakati wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya elimu ya msingi na huku wa tatu ukiwa ni ule unaouhusu uteuzi wa viongozi wa elimu katika mamlaka za serikali za mitaa na mikoa.
Aidha, Mhanze alisema miongozo yote mitatu ambayo imezinduliwa inaenda kufanya kazi kwenye kila ngazi husika kuhusiana na suala zima la elimu
“Katika ngazi ya halmashauri sio watu wa elimu tu wanaweza kujitegemea, ila idara zote zikitoa huduma stahiki na kwa ufanisi mkubwa utekelezaji wa miongozo hii utakwenda vizuri,” alisema Mhanze.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.