SHIRIKA lisilo la kiserikali la Child Support Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Christian Blind Mission wamekabidhi msaada wa baiskeli {Viti Mwendo} 5 za walemavu katika shule ya msingi Kibaoni halmashauri ya wilaya ya Chunya.
Msaada huo umelenga kuwawezesha wototo wenye ulemavu kuweza kukabiliana na changamoto zinazo wasababisha wasipate Elimu kwa ufasaha.
Akikabidhi msaada huo leo wenye thamani ya milioni 2.2 Mkurugenzi mtendaji wa Child support Tanzania Bi. Noelah Msuya amesema wao kama shirika wamejikita kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata elimu katika mfumo wa Elimu jumuishi.
Amesema nia yao kubwa ni kuhakikisha wanaondoa vikwazo vinavyo wasababisha waototo wenye ulemavu wasipate elimu kwa ufasaha
“Nia yetu kubwa ni kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata elimu katika mazingira salama na yenye ubora” alisema Bi Noelah Msuya Mkurugenzi mtendaji wa CST.
Vile vile shirika la Child support Tanzania limekuwa likitoa elimu kwa makundi mbalimbali kuhusu ulinzi na haki za watoto
Bi Noelah Msuya amewataka wazazi wanaopata elimu kuhusu haki za watoto kuhakisha wanaeple elimu hiyo kwa jamii ili kuhakikisha watoto wanakuwa katika mazingira salama .
Kwaupande wa Bw. Richard Dallu Program officer wa Christian blind mission Tanzania amesema wao lengo ni kuhakikisha jamii inakuwa jumuishi.
Tumekuwa tunafanya kazi na wadau mbalimbali wakiwamo CST kupitia hao wadau wanaenda kugusa maisha ya watoto hasa wenye ulemavu
Pia ametumia fursa hiyo kuwahasa wazazi wa watoto waliopewa msaada wa viti mwendo kuhakikisha wana vitunza vizuri na kuendelea kuwasaidia watoto wao.
“Viti mwendo ambavyo tunawapatia tunaomba sana muweze kuvitunza ili viweze kuendelea kuwahudumia watoto vizuri” amesema Bw. Richard Dallu
Naye Afisa Elimu Maalum wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi. Hawa Mtonyole amewashukuru shirika la Child support Tanzania kwa kushirikiana na Christian Blind Mission kwa msaada wa viti mwendo walivyotoa kwa watoto wenye ulemavu katika shule ya msingi kibaoni
Aidha ameyaomba mashirika hayo kuendelea kutoa misaada hiyo kwakuwa wahitaji bado ni wengi sana ndani ya chunya na uhitaji wa viti mwendo ni mkubwa sana.
Sambamba na hayo Bi. Mtonyole ameiomba Serikali,wadau na taasisi mbalimbali zinazo wazunguka kuweze kusaidia kuboresha miundombinu ya shule ya msingi kibaoni ili iweze kuendana na kukidhi mahitaji ya Elimu Jumuishi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Child Support Tanzania Bi. Noelah Msuya akizungumza wakati wa utoaji wa msaada wa viti mwendo kwa wanafunzi wenye ulemavu shule ya msingi Kibaoni
Afisa Elimu Maalumu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi. Hawa G Mtonyole akizungumza wakati wa halfa ya utoaji wa msaada wa viti mwendo kwa wanafunzi wenye Ulemavu katika shule ya msingi kibaoni
Wawakilishi wa Child Support Tanzania, wawakilishi kutoka Christian Blind Mission wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wenye ulemavu mara baada yakupewa msaada wa viti mwendo
Ndugu Richard Dallu Program Officer wa shirika la Christian Blind Mission Tanzania akizungumza katika halfa ya utoaji wa msaada wa viti mwendo kwa wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi kibaoni
Ndugu Yusuph Libaba Mwenyekiti wa kamati ya shule ya Msingi Kibaoni akitoa neno la Shukrani kwa shirika la CST kwa msaada waliotoa wa viti mwendo kwa wanafunzi wenye ulemavu katika shule hiyo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.