Meneja uendeshaji wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tumbaku Chunya (CHUTCU) Ndugu Juma Shinshi amesema wamejipanga kuanza ziara ya siku mbili kuhamasisha wakulima wananchama wa Chama hicho kujiandikisha wao, familia zao pamoja na vijana wanaowasaidia kutekeleza shughuli za kilimo cha Tumbaku ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya huku lengo likiwa ni kuungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha suala la Uchaguzi linafanikiwa
Akizungmza ofisini kwake mapema leo tarehe 15/10/2024 Shinshi amesema kuanzia Kesho uongozi wa Chama kikuu cha Ushirika watakuwa na ziara ya kuhamasisha wakulima wananchama wake pamoja na wananchi wengine wote wajitokeza kujiandikisha kwenye Daftrai la mkazi la kitongozi ili kujipatia sifa ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotaraji kufanyika Novemba 27, 2024 nchini kote
“Sisi Chama Kikuu cha Ushirika cha Tumbaku Chunya (CHUTCU) Tunaungana na Serikali kwenye suala la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo leo tarehe 15/10/2024 wafanyakazi wote wataenda kujiandikisha kwenye vituo vya kujiandikishia kwa kuzingatia maeneo na vitongoji wanavyoishi lakini kuanzia kesho (16/10/2024) tutakuwa na ziara ya siku mbili kuwapitia wakulima wanachama wetu ili kuwahimiza kujiandikisha na baadaye wajitokeze kupiga kura kwa mujibu ya ratiba zinazotolewa” amesema Shinshi
Aidha, Shinshi ameongeza kuwa taasisi nyingine za Serikali na hata taasisi zisizo za serikali zinapaswa kuhakikisha wananchi (watumishi) wao wanajiandikisha lakini wanajitokeza kupiga kura kipindi cha Kupiga kura kitakapofika kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamewatendea haki wafanyakazi wao lakini pia watakuwa wamemuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Bi Rehema Sanga, Ndugu Francisco Chidege, Bi. Hilda Shauritanga, Ndugu Abdalah Ndunya pamoja na Bi Elina Kadunda (Baadhi ya watumishi wa CHUTCU) wamesema wanaushukuru uongozi wa CHUTCU kwanza kuwaruhusu kwenda kujiandikisha kila mmoja kwenye kituo chake lakini pia kuwapatia usafiri wa kuwapeleka kwenye vituo hivyo ili kurahisisha zoezi hilo huku wakidai jambo hilo linafaa kuigwa na taasisi nyingine.
Zoezi la uandikisha wapiga kura kwenye Daftari la mkazi la Kitongozi lilianza rasmi tarehe 11/10/2024 na litatamatika tarehe 20/11/2024 hivyo wananchi wanaaswa kutumia vema muda wa siku tano ulio salia na kwa kufanya hivyo watakuwa wametekeleza katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia wanakuwa wameitumia vizuri haki yao ya msingi
“Serikali za Mitaa, Sauti ya wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi”
Bwana Francisco Chidege akitia saini kwenye Dfatrai la Mkazi la Kitongoji cha Sinjilili A anakoishi ikiwa ni baada ya kukamilisha kujiandikisha Mapema leo tarehe 15/10/2024 katika kituo cha kuandikishia wapiga kura kilichopo Idara ya Maji
Bi Hilda Shauritanga (Mfanyakazi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tumbaku Chunya (CHUTCU) akikamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye Kitongoji cha Sinjilili A eneo analoishi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.