Halmashauri ya wilaya ya Chunya imevukaa lengo kwa asilimia 6.92 katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2022/2023 na kupelekea halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza kati ya halsmhauri zote saba za Mkoa wa Mbeya
Hayo yamesemwa leo Septemba 01/2023 wakati wa Mkutano wa baraza la madiwani kwa robo ya nne ( 4 ) ambapo baraza hilo limepokea na kujadili taarifa mbalimbali za kamati na kupiti utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Makusanyo ya jumla ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuanzia mwezi julai hadi Juni 30/2023 ambayo ni sawa na aslimia 106.92 ambapo makusanyo yaameongezeka kwa asilimia 6.92 ya lengo la makisio ya mwaka” Alisema mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mhe Bosco Said Mwanginde
Kupitia ongezeko la Ukusanyaji wa Mapato Baraza la Madiwani limeazimia kuwapa motisha wakusanyaji wa mapato na kuitaka Halmashauri kuongeza juhuddi zaidi katika ukusanyaji wa Mapato ili kuiwezesha Halmashauri kuwa na vyanzo vingi zaidi vya mapato na si kutegemea ushuru pekee.
‘’Tuhakikishe tunaongeza juhudi katika ukusanyaji wamapato ili turudi katika nafasi ya kwanza tufanye vizuri zaidi na kuvuka malengo kwasababu tukikusanya vizuri mapato itasaidia kuongeza utekerezaji wa miradi kupitia vyanzo vyetu vya ndani lakini pia kubaini vyanzo vngine vitakavyosaidia ongezeko la mapato’’ alisema Mhe. Bosco Mwanginde” Aliongeza Mhe Mwanginde
CPA Eliah Chigoji akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameitaka Halmashuri kuongeza Juhudi zaidi katika ukusanyaji wa mapato hali itakayochangia Halmashauri kuwa na Vyanzo vingi vya mapato vitakavyochangia Halmashuri kuendelea kuongoza katika ukusanyaji wa mapato
“Niwaombeni tuongeze nguvu ili sasa yale mapato tunayoyakusanya tukazidi kuibua vyanzo vingi vya mapato ili siku za usoni tuwe na vyanzo vingivya mapatao tusitegemee ushuru peke yake”
Katibu tawala wilaya Chunya akimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Chunya amewapongeza madiwani pamoja na watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya chunya huku akisema mafanikio ya wilaya ya Chunya yanatokana na ushirikiano uliopo kwa viongozi kwa ujumla, hivyo amewataka wajumbe wa kikao hicho kuendeleza ushirikiano huo ili Chunya iendelee kufanya vizuri
Akitoa salamu katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Chunya Lutufyo Mwambugu amewataka madiwani na Halmashauri kwa ujumla kuendelea kutengeneza misingi mizuri ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato pia amewaomba Madiwani kuwa sehemu ya Utekelezji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao kwa kushirikiana na wataalam ili kuhakikish miradi hiyo inayotekelezwa ina kuwa ya viwango.
Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa robo ya nne (4) uliotakiwa kuketi tarehe 28/7/2023 umefanyika leo septemba mosi, 2023 na kuhudhuriwa na waheshimiwa Madiwani, Mwakilishi wa Mkuu Mkoa , mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya , Katibu wa chama cha Mapinduzi, Wataalamu, Vyombo vy Ulinzi na Usalama, Waandishi wahabari na Wananchi
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wilaya ya Chunya wakiwa katika kikao cha Baraza la madiwani kwa robo ya nne ya mwaka 2022/2023
Mhe Ramadhan Shumbi Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya akisoma taarifa ya kamati ya uongozi fedha na mipango (FUM) kwa wajumbe wa kikao cha Baraza la Madiwani kwa robo ya nne ya mwaka 2022/2023
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.