Halmashauri ya wilaya ya Chunya imejipanga kushirikisha jamii kuibua na miradi ya maendeleo yenye maslahi mapana kwa jamii jambo litakalo hakikishia ulinzi na usalama wa miradi hiyo kwani jamii yenyewe ndio itakayohusika kuanzisha miradi hiyo, kutekeleza mpaka ukamilishaji wake pamoja na kuilinda.
Akizungumza leo 29/09/2023 kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo ulioboreshwa (Opportunities and Obstacles for Development (O & OD)) ndugu Nebart Gavu amewataka washiriki kwenda kupeleka Elimu waliyoipata kwa wananchi ili wananchi moja kwa moja washiriki zoezi la kuibua miradi ya maendeleo yenye maslahi kwao na kuwashirikisha katika utelekezaji wa miradi hiyo huku akihimiza uwajibikaji na uwazi wa taarifa kwa kila hatua za utekelezaji wa miradi hiyo.
“Ndugu washiriki serikali imewaamini ninyi kuwa wawezeshaji wa mpango wa fursa na vikwazo kwa jamii na ni matumaini yetu mafunzo mliyoyapata yatawafikia wanajamii na yataleta mapinduzi chanya katika Maendeleo ya wanajamii. Pia Mafunzo haya yamewapa mwongozo ninyi wa namna sahihi ya kutekeleza majukumu yenu na namna sahihi ya kuishirikisha jamii katika miradi yote inayoibuliwa na kutekelezwa katika jamii na jambo muhimu ni ukweli na uwazi na uwajibikaji kwa kila hatua za mradi” alisema Ndugu Gavu
Aidha Ndugu Gavu amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuendelea kutekeleza mkataba wa lishe kwakuwa suala la Lishe sasa ni jambo la kitaifa na amesema ili jamii iweze kushiriki kikamilifu katika uibuaji wa miradi pamoja na utekelezaji wa miradi hiyo ni lazima jamii hiyo iwe na afya njema hivyo lishe ina nafasi kubwa kwa jamii kushiriki kikamilifu katika suala la maendeleo.
“Suala la Lishe linaendelea na ni wimbo wa Taifa kwasasa hivyo endeleeni kutazama hilo na kutekeleza mkataka wa lishe na tunategemea mapinduzi makubwa katika maeneo mbalimbali mnayoyasimamia ikiwepo suala la Lishe”
Kwa niaba ya washiriki wote mtendaji wa kata ya Sangambi ndugu Mtundu Chapa ameshukuru serikali kuwapatia mafunzo hayo ambayo yana nafasi kubwa kusaidia utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na ameahidi kwa niaba ya washiriki wenzake kwamba watayatendelea kazi mafunzo hayo ili kuhakikisha wananchi wanafaidika kwa uwepo wao katika vijiji na kata wanazotoka. Aliongeza Ndugu Gavu
Mafunzo hayo yaliyoshirikisha watendaji wa vijiji na kata, maafisa ugani na maafisa maendeleo ya jamii ambao jumla yao ni 92 yamehitimishwa rasmi leo tarehe 29/09/2023 kwa maafisa kutoka tarafa ya kiwanja kuhudhuri mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo)
Paul Lugodisha (Aliyesimama Mbele kushoto) akiendelea na uwezeshaji wakati wa mafunzo ya Mfumo wa fursa na vikwazo ulioboresha katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo), waliokaa ni washiriki wa mafunzo kutoka Tarafa ya kiwanja
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika makundi ili kupima uelewa wa kile walichojifunza wakati wa mafunzo, baadhi ya waliosimama ni wakufunzi wa mafunzo hayo wakipitia kundi moja baada ya kundi lingine ili kuona washiriki wanavyoonesha uwezo wao juu ya kile walichojifunza
Mtendaji wa kata ya Makongolosi Ndugu Egithol Bilal (Aliyenyoosha Mkono kuielekea karatasi iliyoshikwa kikamilifu na washiriki wawili wa nafunzo) akielezea namna kundi lake lilivyotengeneza mpango kazi wa maendeleo kuzingatia ushirikishwaji wa jamii ikiwa ni kupima uelewa wa mafunzo waliyopatiwa mapema leo
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo wakiendelea kufuatilia mafunzo kwa ukaribu na alyesimama nyuma yao ni moja kati ya wawezeshaji wakiendelea kuhakikisha washiriki wanapata kile kilichokusudiwa kwa uafasaha
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.