Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bingwa mtetezi wa mchezo wa kuvuta Kamba SHIMISEMITA msimu uliopita msimu huu bado inaendelea kuwabuluza wapinzani wake katika michezo ya watumishi inayoendela jijini Dodoma baada ya Timu ya wanawake kuvuta Kamba kuingia nusu fainali wakati Timu ya wanaume kuvuta kamba iko Robo Fainali
Chunya DC Vs Moshi DC (ME) mshindi CHUNYA DC
Chunya DC Vs Tunduma TC (KE) mshindi CHUNYA DC
Kwa matokeo hayo Chunya Dc wanaume wametinga hatua ya robo fainali (Mtoano) ambapo watakutana uso kwa uso timu ya watumishi kutoka Arusha jiji huku timu ya Chunya DC wanawake wao wametinga hatua ya nusu fainali ambapo watavaa na timu Kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam (DAR CC) ambayo ni kesho asubuhi.
Kuelekea Mchezo wa Nusu Fainali kepten wa timu ya wanawakeChunya DC Kuvuta kamba Bi Devotha Mwasaga amesema kilichobaki kutoka kwa wanachunya ni dua, Sara na Maombi ili kufanikisha azma ya kuleta ushindi Chunya na hatimaye kuiheshimisha wilaya ya Chunya kwani upande wa Maandalizi hakuna changamoto yoyote timu iko salama.
“Tunachokihitaji kutoka kwa wananchunya ni maombi kila mmoja kwa Imani yake ili timu iweze kufanikiwa kutwaa ubingwa kwani upande wa maandalizi kila kitu kiko vizuri, wachezaji wana ari na morali wa kuhakikisha ubingwa unakuja Chunya hivyo tuiheshimishe Chunya yetu”.
Kwa upande wa timu wanaume kuvuta kamba kepteni wa Timu hiyo Ridhiwani Mshigati amesema bado timu iko Imara na iki tayari kwa michezo yote iliyo mbele yetu huku lengo ni lile lile kuchukua tena ubingwa katika mashindano hayo hasa kwa upande wa Mchezo wa Kuvuta Kamba.
“Kwenye mchezo wa kuvuta kamba tumeendelea na kutetea ubingwa wetu na ndo maana tumeshinda 2 bila kwa maana ya kwamba tuliocheza nao tumefunga awamu zote mbili, na kamba ina mbinu za kupata ushindi, sisi tumehatika kupata mtaalamu anatuongoza vizuri na kwasasa tuko kambini tunaendelea kupeana mbinu na kutunza nidhamu. kurudi mikono mitupu kwa Mwajiri ni aibu kubwa ambayo sisi hatutaki itokee kwetu kulingana na huduma tulizopewa na mwajili wetu.
Na tunashukuru Halmashauri jirani za Rungwe na Tunduma wanatusapo, ingawa Tunduma Tc walifungwa na timu ya wanawake kuvuta kamba tuliwaomba radhi na kuwambia kwa hili hatuna ujirani tukawatoa, Tunaomba watu wa Chunya waendelee kutuombea ili kutetee ubingwa wetu na lengo ni siku ya kufungwa kwa Mashindano haya Halmashauri yetu ya Chunya Itajwe na Mgeni rasmi na Bendera yetu iweze kupepea mbela ya Halmashauri zaiidi ya Mia moja zilizoshiriki Mashindano hayo” amesema Mshigati.
Utofauti wa hatua yaani Timu ya wanaume kuwa hatua ya Robo Fainali (Mtoano) huku timu ya wanawake kuwa hatua ya Nusu Fainali umetokana na Idadi ya timu zilizoshiriki mchezo huo kwani Timu za wanawake zilikuwa chache kulinganisha na timu za wanaume hivyo kupelekea kupelekea baadhi ya hatua za mashindano kuwa na mzunguko mfupi kulingana na timu za wanaume.
Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndiye Bingwa Mtetezi wa Mchezo wa Kuvuta Kamba Taifa kwa msimu wa mwaka 2022 na sasa timu zote ziko hatua nzuri kutetea ubingwa mwaka huu 2023, Maombi, bahati pamoja na kujituma vitaendelea kuhitajika ili timu zetu ziendelee kufanya vizuri
Timu ya wanaume kuvuta kamba ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ikiongozwa na Kepteni mwenye Nidhamu na Maadili Bw Ridhiwani Mshigati ikiendelea kuwabuluza wapinzani wake kwenye Mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea Jiji Dodoma
Timu ya wanawake ya kuvuta Kamba ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ikiongozwa na Kiongozi mwanamama mwenye misuli Bi Devotha Mwasaga ikiendeleza ubabe wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Jijini Dodoma
Timu ya wanaume kuvuta Kamba ikisubiri maelekezo kuchukua pointi zote kwenye michezo yao inayoendelea huko Dodoma, Aliyeshika kiuono wa pili kutoka Kushoto ni Kepteni wa Timu hiyo Bwana Ridhiwani Mshigati ikihimiza jambo kwa wenzake
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.