Halmashauri ya wilaya ya Chunya kupitia viongozi wake imeanza mchakato wa kufanya biashara ya Hewa Ukaa ili kuongea uwezo wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuingiza mapato na hatimaye kuendelea kuongoza katika ukusanyaji wa mapato ndani ya Mkoa lakini kuendelea kutekeleza miradi ya Maendeleo yenye lengo la kusogeza huduma kwa wananchi wa Chunya ili waendelee kuifurahia serikali ya awamu ya sita
Katika kutimiza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mh. Bosco S. Mwanginde ameongoza msafara wa Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipngo kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ambayo tayari ni mnufaika wa Biashara hiyo ambapo mpaka sasa miradi mbalimbali ya maendeleo imejengwa kwenye wilaya hiyo kutokana na biashara ya hewa ukaa (Biashara ya Kaboni)
Katika ziara hiyo iliyohusisha waheshimiwa Madiwani wajumbe wa kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango (FUM) pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ililenga kupata ufahamu wa kina kuhusu mchakato mzima wa Biashara ya Hewa Ukaa (Biashara ya Kaboni) na baadaye kuona namna ambavyo Halmashauri ya wilaya ya Chunya itaweza kujihusisha na biashara hiyo ambayo pamoja na kujipatia fedha lakini pia itaongeza usimamizi na utunzaji wa Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Miradi iliyotekelezwa kwa fedha zitokanazo na biashara ya Hewa Ukaa (Biashara ya Kaboni) Keiyer Ilikiush Afisa Mipango na uratibu ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya WMA “Kadiri miaka inavyoongezeka ndivyo kaboni inavyozidi kuongezeka na kadiri Kaboni inavyoongezeka ndivyo wilaya ya Kiteto inavyozidi kupata faida
Kupitia fedha hizo miradi mbalimbali katika wilaya ya Kiteto imetekelezwa huku wanaofaidika zaidi ni vijiji wenye mradi
-Madarasa zaidi ya 17 yamejengwa katika vijiji vitatu kupitia fedha zinazotokana na Biashara ya Hewa ukaa (Kaboni)
-Nyumba ya walimu ya Mbili katika moja (Two in one) imejengwa kupitia fedha hizo
-Jengo la Mama na Mtoto lenye hadhi ya kituo cha Afya limejengwa kwenye zahanati ya kata ya Makame
-Ofisi ya Kijiji cha Kata vimejengwa kwa fedha za hewa ukaa
-Bweni lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 80 kwenye shule ya sekondari ya tarafa ya Makame limejengwa kwa fedha za hewa ukaa
-Zaidi ya wanafunzi 200 kutoka maeneo ya mradi wamesomeshwa kwa kufadhiliwa na fedha zinazotokana na mradi huo
-Maabara za kisasa zimejengwa kwenye vituo vya Afya kupitia fedha zitokanazo na mradi Hewa ukaa (Mradi wa Kaboni)
-Ofisi za kata na vijiji hupata fedha za kuendeshea ofisi kutoka kwenye mradi Hewa ukaa (Mradi wa Kaboni)
Diwani wa kata ya Makame Mhe Issaya Kilaye Ndutui amewashauri viongozi na msafara mzima toka wilaya ya Chunya kwamba kabla ya Biashara hii kuanza kuingiza fedha ni muhimu mpango wa matumzi ya fedha hizo ukawekwa ili fedha zikipatikana ni kuendelea kutekeleza mpango husika jambo hilo husaidia uwazi wa matumzi ya fedha
Naye diwani wa kata jirani na Makame Mhe Paulo Yohana Laizer amesema kupitia mradi wa biashara ya Hewa Ukaa kila kijiji wamenunuliwa dume bora la Ng’ombe, wamepatiwa Milioni tabo ambazo ni nje ya mkataba, wananchi mia moja kutoka kila kijiji kinachonufaika na mradi wa Biahsra ya Hewa ukaa wamelipiwa Bima ya Afya hivyo amewashauri kamati ya fedha Uchumi na Mipango kuenda kuona namna bora ya kuingia kwenye biashara hii kwani inafaida nyingi kwa wananchi
Mhe Ramadhani Shumbi, Mh. Weston S. Mpyila, Mh. Phide K. Mwalukasa ni baadhi ya waheshimiwa Madiwani waliouliza Maswali Mbalimbali wakati upande wa wataalamu, Dkt Lucas Theodory, Bi Simphrose Kavishe na wengine pia waliuza Maswali mbalimbali na kupatiwa ufafanuzi na wataalamu kutoka wilaya ya Kiteto
Baada ya Mafunzo na maelekezo ya Baishara ya Hewa ukaa (Biashara ya Kaboni) Mwenyekiti waHalmashauri ya wilaya ya Chunya kwa Niaba ya msafara Mzima aliwashukuru wenyeji wa kata ya Makame na uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa namna walivyowapokea lakini pia kwa elimu waliyowapatia pia aliwataka kuendelea kuwa wavumilivu pale Chunya itakapowahitaji kwa maelekezo na mahusiano zaidi wasisite kuwasikiliza na kuwasaidia
Biashara ya Hewa Ukaa nini basi?
Biashara ya Hewa ukaa wakati mwingine Huitwa Biashara ya Kaboni ambapo mtu binafsi, kijiji, Halmashauri na taasisi nyingine yoyote inaweza kuanza kupata kuingiza fedha kwa kuamua kutenga msitu na kuutunza kiasi cha kusaidia kupunguza hewa mbaya (Carbon dioxide) inayopatikana huku angani
Kupitia Biashara hiyo Halmashauri ya wilaya ya Kiteto imepata faida tofauti tofauti ambapo kwa kila mwaka kiwango cha fedha wanachopata huongezeka kutokana na uwezo wa kutunza na kutokukata miti katika misitu tengwa kuendelea kuimarisha mfano mwaka
-2020/2021 walipata Milioni sitini (60)
-2021/2022 walipata bilioni moja na milioni miatatu
-2022/2023 wamepata bioni mbini na milioni mia tano
Biashra hii imeshaingia katika Mikoa mbalimbali ikiwepo mkoa wa Katavi, wilaya ya Tanganyika ambapo wananchi zaidi ya 21,000 katika vijiji 8 walio katika Halmashauri ya Tanganyika wamenufaika na mradi wa hewa ukaa baada ya kuvuna hewa hiyo na kupewa kiasi cha shilinmi milioni mia tatu na themanini elfu (380,000,000/=)
Walichofanya wananchi katika wilaya hiyo ni kuzuia uharibifu wa mazingira katika misitu waliyoihifadhi ili iwasaidie kuvuna hewa ya kaboni na hatimaye kujiingizia kipato baada ya hewa iliyovunwa kuuzwa/kufidiwa na makampuni kutoka nje ya Nchi
Kwa ufafanuzi zaidi vijiji hivyo kutoka Halmashauri ya Tanganyika vimevuna jumla ya tani 82,000 za hewa ya kaboni na kuiuza kwa thamani ya shilingi milioni mia mbili na hamsini (250,000,000/=) hata hivyo pamoja na uvunaji watani hizo, mauzo yake hayajafikia hata nusu ya tani laki mbili na sabini (270,000/=) ambazo bado hazijauzwa
Aidha mwaka 2020 zaidi ya shilingi milioni mia moja na thelasini zilitolewa kwa viji wanufaika wa mradi kama motisha na wadau mbalimbali wa mazingira ambazo ni nje ya makubaliano ya biashara ya hewa ukaa
Tafiti zinaeleza kwamba katika vijiji hivyo vya wilaya ya Tanganyika kuna utajiri mkubwa wa misitu hivyo kama itasimamiwa vizuri kuna uwezekano wa kupata pesa zaidi ya bilioni sita (6,000,000,000/=) kutokana na biashara ya hewa ukaa
Mkoa wa Iringa pia uko katika biashara hii ya hewa ukaa ambapo vijiji vinne kutoka wilaya ya Mufindi vilipata milioni mia mbili na themanini mwaka 2021 kutokana na biashara ya hewa ukaa(Biashara ya kaboni) ambapo fedha hizo zilisaidia maendeleo ya wananchi katika vijiji hivyo. Vijiji vilivyonufaika na fedja hizo ni Kijiji cha Uchindilele shilingi milioni 140, Kijiji cha Mapanda shilingi milioni 67.4, kijiji cha Chogo Shilingi Milioni 64.4 na kijiji cha Kitete shilingi milioni 8.4
Swali linabaki kwako Mwananchi wa Chunya
Endelea kuiamini Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika wilaya ya Chunya akisaidiwa na viongozi kama vile Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chunya na vyombo vyake, Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mhe Bosco S Mwanginde, Watendaji wa serikali wakiongozwa na Ndugu Tamimu Kambona Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Elimu kuhusu biashara ya hewa ukaa itaendelea kukufikia kupitia mitandao yetu ya halmashauri ya wilaya ya chunya
Lazaro C. Rinjano afisa Maliasili wilaya ya Kiteto akitoa salamu za ukaribisho kwa msafara wa Waheshimiwa Madiwani wajumbe wa kamati ya FUM pamoja na viongozi mbalimbali kutoka wilaya ya Chunya walipowasili Halmashauri ya wilaya ya kiteto
Diwani wa kata ya Ndedo Mhe Paulo Yohana Laizer akifafanua jambo mbeya ya Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati msafara kutoka wilaya ya Chunya ukiwasili makao makuu ya mradi wa WMA tayari kupata elimu kuhusu Hewa ukaa (Kaboni). Misitu inayoonekana kuzunguka eneo hilo ndiyo aina ya misitu ambayo huwapatia faida kupitia hewa ukaa (Biashara ya Kaboni)
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco S Mwanginde akitoa salamu za wilaya ya Chunya kwa viongozi wa Wilaya ya Kiteto (Hasa Eneo la Mradi) na akifafanua lengo la safari hiyo kwenye wilaya ya Kiteto
Diwani wa kata ya Makame (Eneo ambalo linaendesha mradi wa Hewa ukaa) Mhe Issaya Kilaye Ndutui akifafanua jambo kwa viongozi toka wilaya ya Chunya kabla ya kuanza mafunzo kuhusu Elimu ya Hewa Ukaa (Biashara ya Kaboni) na namna inavyowanufaisha wananchi wa kata hiyo
Afisa mipango wilaya ya Kiteto ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Bodi ya mradi wa WMA Ndugu Keiyer Ilikiush akitoa Elimu kuhusu mradi wa Hewa Ukaa (Biashara ya Kaboni) na namna wilaya ya Kiteto ilivyofaidika tangu walioanza kutekeleza mradi huo
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Ramadhan Shumbi (Aliyesimama na amenyoosha mikono mbele) akiuliza jambo kuhusu Hewa ukaa huku akieleza namna alivyokuwa anaelewa kuhusu Hewa Ukaa kabla ya kupatiwa mafunzo
Diwani viti maalumu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mh. Phide K. Mwalukasa akiuliza swali kuhusu aina ya misitu inayohusika kwenye mradi na pia ulazima wa misitu kuwa eneo moja
Diwani wa kata ya Ifumbo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mh. Weston S. Mpyila akiuliza swali la uelewa wakati wa mafunzo kwa viongozi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya yanayohusu biashara ya Hewa ukaa (Biashara ya Kaboni)
Katibu tawala wilaya ya Chunya Ndugu Anakleth Michombero akifafanua jambo wakati wa mafunzo kuhusu Hewa ukaa wakati wa ziara ya viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kujifunza Wilayani Kiteto
Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Dkt Lucas Theodory akiuliza jambo wakati wa Mafunzo kuhusu biashara ya Hewa Ukaa (Biashara ya kaboni) wakati wa Ziara ya Mafunzo wilayani Kiteto
Bi Simphrose Kavishe mtaalamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya akihoji jambo wakati wa Mafunzo kuhusu Hewa Ukaa wakati viongozi wa wilaya ya Chunya walipotembelea wilaya ya Kiteto ili kujifunza kuhusu Hewa Ukaa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.