Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Lupa, Chunya Ndugu Cutherth George Mwinuka amewaonya wasimamizi wa Uchaguzi ngazi za vituo kutotumia Uzoefu wao katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025 bali wazingatie Sheria Kanuni na Utaratibu pamoja na maelekezo yanayotolewa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru, haki na amani
Ametoa kauli hiyo mapema leo 26.10.2025 wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi za vituo walioteuliwa na tume, mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Lupa.
“Naomba kuwaonya wasimamizi wazoefu ambao wamesimamia uchaguzi mara nyingi kwani kuna mambo mengi yamebadirika hivyo zingatieni Mafunzo kama mtakavyoelekezwa lakini pia pitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya Uchaguzi yam waka 2024, miongozo na Maelekezo kadiri yatakavyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi”
Aidha Mwinuka amewataka wasimamizi wa vituo wote pamoja na watumishi wengine kwa mujibu wa miongozo ya tume huru ya Taifa ya Uchaguzi watakaokuwepo eneo la kituo cha kupiga kura wazingatie weledi na nadhifu wa mavazi wakati wa zoezi kwa ujumla
Akihitimisha hotuba yake Ndugu Mwinuka amewakumbusha washiriki wa Mafunzo wote kuachana na matumizi ya simu janja siyohitajika na Tume kwa ujumla kwani matumizi ya simu yanaweza kukusababishia ubize usio na maana wakati wa zoezi au kuitumia simu janja hiyo inaweza kutumika kinyume cha maelekezo ya tume
Semina kwa wasimamizi na watendaji wa vituo katika Jimbo la Lupa imeanza jana kwa makarani waongozaji, huku leo tarehe 26.10.2025 ikiwa ni semina kwa wasimamizi wa vituo pamoja na wasimamizi wa wasaidiizi na semina itakayodumu kwa siku mbili lengo likiwa ni Uchaguzi huru na wa haki

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Lupa Bwana Cuthberth Mwinuka akizungumza na wasimamizi wa vitu wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo mapema leo 26.10.2025 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Lupa

Washiriki wa Mafunzo wakisikiliza kwa makini Hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo Mapema leo, Mafunzo yanayofanyika kwa siku mbili

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Lupa wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.