Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Dkt Darison Andrew kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Chunya amesema lengo la Halmashauri ya wilaya ya Chunya ni kushika nafasi ya Kwanza kitaifa katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ili kuendelea kuwahakikishia wananchi wa Chunya usalama wa afya ili waendelee kujihusisha na uzalishaji mali bila shaka yoyote.
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 24/10/2023 wakati alipoongoza kikao cha Lishe kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 kilichoketi ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya uliopo jengo jipya la utawala kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji ambapo amewataka idara mbalimbali zilizo chini ya ofisi ya Mkurugenzi mtendaji kujipanga kwa namna zote ili kufanikisha azma hiyo.
“Matamanio yetu Halmashauri ya wilaya ya Chunya ni kushika nafasi ya kwanza Kitaifa katika utekelezaji wa mktaba wa Lishe hivyo lazima tujipange kuhakikisha tunatimiza azma hiyo na ili tutumize azma hiyo lazima tushirikiane kwa pamoja kuanzia sisi mpaka mtu wa mwisho kabisa katika Mnyororo wa Lishe ambaye ni mwananchi”.
Aidha Dkt Andrew amewataka mafiasa Elimu Msingi na Sekondari kusimamia suala la Chakula shuleni kwani utoaji wa Chakula Shuleni ni agizo la Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mtu anayekaidi kuleta chakula shule ili watoto wapate chakula wawapo shuleni maana yake anakiuka maelekezo ya Rais hivyo achukuliwe hatua kali kwa mujibu wa Sheria.
Akitoa taarifa mbele ya Kikao hicho Afisa Lishe Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi Rehema Hiluka amemshukuru Mkurugenzi mtendaji kwa namna ambavyo amehakikisha fedha zote zilizopangwa kwaajili ya utekelezaji na usimamizi wa wa lishe zinatolewa kama bajeti inavyoelekeza na pesa hizo zinatolewa kwa wakati.
“Pamoja na kutoa taarifa za kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe Kitaifa ambapo wilaya ya Chunya ilishika nafasi ya tatau kitaifa lakini naomba kipekee nikushukuru Mkurugenzi kwa namna ambavyo unahakikisha fedha zilizopangwa kwaajili ya kutekeleza mkataba wa Lishe zinatolewa na pia zinatolewa kwa wakati sahihi. Na kwa robo hii ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 tumepokea fedha zaidi ya lengo ambapo tumepokea asilimia 126 ya fedha zilizotakiwa kwutekelezaji wa mkataba wa lishe kwa Robo hii ya kwanza ya mwaka”.
Kikao cha Lishe kimeketi leo tarehe 24/10/2023 ikiwa ni kikao cha Lishe kwa Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 na huwa kinakaa kila robo ya mwaka wa fedha kutamatika lengo ikiwa ni kutathimini mwenendo wa lishe kwa robo husika, kama kuna changamoto za utakelezaji wa mkataba wa lishe hutafutiwa suluhu katika vikao hivyo
Afisa Lishe wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi Rehema Hiluka akitoa taarifa wakati wa kikao cha Lishe kwa Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 kilichoketi leo ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya uliopo jengo jipya la utawala
Bi Komba akimuwakilisha Afisa Elimu sekondari akichangia namna ambavyo idara ya Elimu sekondari itakavyofanikisha suala la lishe kwa wanafunzi wa sekondari kwa Robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023/2024 ili kufikia nafasi ya kwanza kitaifa kama ilivyo azma ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Dkt Benedict Matogo akichangia hoja kwenye kikao cha Lishe mapema leo namna ambavyo Divisheni ya kilimo itakavyoshiriki kuhakikisha wilaya ya Chunya inapata nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa Mkata wa Lishe kitaifa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.