Vijiji 43 na vitongoji 233 kutoka kata 20 na tarafa mbili za Halmashauri ya wilaya ya Chunya kushiriki uchaguzi wa Kupata viongozi wa vijiji na vitongoji katika uchaguzi unaotaraji kufanyika Novemba 27, 2024 huku nchi nzima vijiji 12,333, vitongoji 64,274 na mitaa 4,269 uchaguzi utafanyika ili kupata viongozi wa kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya mnahimizwa kushiriki uchaguzi huo ili kuhakikisha Chunya inapata viongozi bora watakaopewa dhamana ya kutuongoza kwa kipindi cha miaka mitano mingine kwani viongozi hawa ndio sauti za wananchi katika maeneo husika (Vijiji na vitongoji)
Kumbuka kauli mbiu ya uchaguzi huo ni “Serikali za mitaa, Sauti ya Wananchi; Jitokeze kushirki uchaguzi”
Endelea kutufutilia katika mitandao yetu, taarifa zote kuhusu Uchaguzi utazipata hapa, mjulishe na mwingine kwamba ni haki yake pia kushiriki uchaguzi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.