MKuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Zuberi Homera amesema Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ni Halmashauri pekee inayotaraji kupokea fedha nyingi zaidi za utekelezaji wa miradi ya WASH ukilinganisha na Halmashauri zingine za Mkoa wa Mbeya ambapo itapokea zaidi ya shilling billion 1.3 ikiwa ni kutokana na usimamizi mzuri wa fedha za ujenzi wa miradi hiyo zilizotolewa awali.
Hayo ameyasema tarehe 07/06/2024 wakati akizungumza na Wananchi kwenye Mkutano wa hadhara baada ya kukagua Mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji na vyoo bora (WASH) Zahanati ya Mbugani iliyopo katika kijiji cha Mbugani.
“Mkoa wetu umepokea fedha nyingi sana zaidi ya bilioni 3 .3 kwaajili ya miradi hii ya WASH na Halmashauri ya Wilaya ya Chunya itapokea fedha nyingi zaidi ukilinganisha na Halmashauri zingine ambapo zaidi ya shilingi billion 1.3 zitapokelewa Chunya kwahiyo niombe tu fedha hizo zisimamiwe vizuri kama mlivyosimamia hapa. Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwakweli wametutoa kimasomaso wao wamefanya vizuri na mambo yanakwenda vizuri”alisema Homera
Aidha ametoa rai kwa kila Halmashauri kuhakikisha inasimamia usafi wa mazingira unaofanyika kila mwezi na kutaka kila kaya kufanya usafi katika maeneo yao ili kuweka mazingira safi na salama ikiwa ni pamoja na kuhakikisha taka ngumu zinakusanywa pembezoni mwa barabara na maeneo yaliyotengwa kwaajili ya kuweka mazingira safi na kujikinga dhidi ya Magonjwa ya mlipuko.
“Taka ngumu zote ziwekwe pembezoni mwa barabara na maeneo yaliyoainishwa ili ziweze kuondolewa na timu ambazo zimeandaliwa kwaajili ya kutoa taka maeneo mbalimbali, Mji wa chunya ni mji ambao unavutia hivyo mtengeneze Mazingira wekeni vifaa vya kuwekea taka (dust bin) kwaajili ya kuweka takataka maeneo mbalimbali ili mtu akija anakuta mji wa Chunya uko safi, tuwe wa mfano kama tulivyokuwa wa mfano katika masuala ya Afya”.alisema Homera
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mhe.Bosco Mwanginde amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania kwa namna anavyowajali wananchi kwa kuendelea kuleta fedha kwaajili ya kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwepo miundombinu ya Afya ambapo Zahanati ya Mbugani imeweza kuboreshewa miundombinu yake na kuwa Zahanati ya kisasa.
Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Dkt Darison Andrew akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji na vyoo bora kwenye vituo vya Afya (WASH) amesema kuwa fedha zilizopokelwa ni shilingi Million 63,233,000/= na nguvu za wananchi zenye thamani ya shilingi Million 3,000,000/= zimesaidia ujenzi wa vyoo vya watoa huduma na wateja, ujenzi wa muindombinu ya maji ujenzi wa tanki la chini la kuhifadhi maji ( underground concrete tank) lenye uwezo wa kuhifadhi lita 30,000 ujenzi wa kichomea taka pamoja na Chumba cha kujifungulia.
Ziara ya kazi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imekagua ujenzi wa Miundombinu ya maji, vyooo na miundombinu mingine katika zahanati ya kijiji cha Mbugani pamoja na kuzungumza na wanachi kwenye Mkutano wa Hadhara katika Zahanati hiyo imeenda sambamba na na kikao cha baraza la hoja za Mkaguzi kilichoketi katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera (wa katikati aliye vaa suti nyeusi) wakati akikagua ujenzi wa mradi wa miundombinu ya maji na vyoo bora katika Zahanati ya kijiji cha Mbugani pomoja na wataalam mbalimbali kutoka ngazi ya Mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Zuberi Homera akinawa mikono katika moja ya miundombinu ya maji liyojengwa katika zahanati ya Mbugani kupitia mradi wa WASH wakati wa kukagua mrradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji na vyoo bora Zahanati hapo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mbugani Mhe. Bosco Mwanginde akitoa shukrani zake kwa Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea miundombinu ya maji na vyoo bora katika Zahanati ya kijiji cha Mbugani.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Zuberi Homera akikagua tanki la chini la kuhifadhia maji (underground concrete tank)lenye uwezo wa kuhifadhi lita 30,000 lililojengwa kupitia mradi wa WASH katika zahanati ya kijiji cha Mbugani
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.