Afisa tawala wa wilaya ya Chunya Bi Semwano Mlawa kwaniaba ya Mkuu wa wilaya ya Chunya amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya kuendelea kujitokeza kuchunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi huku akisisitiza kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo kwa wale wenye maambukizi kwani kupata virusi sio mwisho wa Maisha
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe mosi ya mwezi Desemba ambapo kwa Halmashauri ya wilaya ya Chunya maadhimisho hayo yamefanyika viwanja vya Zahanati ya zamani iliyoko kata ya Makongolosi, Mamlaka ya mji mdogo
“Kwa karne ya sasa Virusi vya Ukimwi sio jambo jipya, kwani kila mmoja wetu anafahamu, hivyo nipo hapa kuwaomba wananchi wa Chunya wote kwanza tuendelee kujitokeza kupima ili kujua maambukizi ya virusi hivyo lakini pia ikiwa umepata maambukizi basi tumia dawa kwani kupata virusi vya Ukimwi sio mwisho wa Maisha” alisema Bi Semwano
Aidha Bi Mlawa amewataka Maafisa wote na jamii nzima kuongeza juhudi kuhakikisha elimu ya VVU inawafikia wananchi wote Pamoja na wanafunzi kupitia klabu zao zilizopo mashuleni kwani kwa kufanya hivyo inaongeza ufanisi wa mapambano ya Ugonjwa huu
Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wilaya ya Chunya Ndugu Anton Denga amesema Halmashauri inatumia njia mbalimbali kuelimisha jamii kuhusu VVU na Ukimwi ili jamii iweze kuwa na uelewa mkubwa na hatimaye kuungana katika mapambano ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi kwa ujumla wake.
Denga amesema wananchi wa Chunya wanafikiwa na Elimu kwa njia za makundi rika, Klabu mbalimbali zilizoko Shule za Msingi na Sekondari, Mikutano mbalimbali ya hadhara Pamoja na makongamano mbalimbali yanayoandaliwa mahusui kwaajili ya kutoa elimu
Afisa Elimu Kata wa kata ya Makongolosi Chunya Bi Rebecca Mkisi amewashukuru wananchi wote Pamoja na viongozi kwanza kuhudhuria kwenye maadhimisho hayo lakini pia kuwa mabalozi wazuri wa yale yaliyozungumzwa kwa wengine ambao hawajafika katika hafla hiyo maadhimisho ya siku ya Ukimwi
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani hufanyika kila Desemba mosi ambapo Halmashauri ya wilaya ya Chunya maadhimisho hayo yamefanyika viwanja vya zahanati ya zamani iliyopo kata ya Makongolosi mamlaka ya mji mdogo, ambapo Pamoja na mambo mengine wananchi waliohudhuria wamepatiwa Elimu ya lishe pia

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushiriki kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya, Viwanja vya zahanati ya zamani kata ya Makongolosi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.