Halmashauri ya wilaya ya Chunya inataraji kufanya vizuri katika mavuno ya zao la Tumbaku msimu wa 2022/2023 kwani Mashamba yanayofanyiwa tathimini na timu ya wadau wa tumbaku mkoa wa Kitumbaku Chunya yanaonesha wazi kwamba hali ya zao shambani ni nzuri
Wakulima kwa nyakati tofauti wamekiri wazi kwamba soko la Tumbaku msimu uliopita limewavutia wengi kuingia katika kilimo na wale waliokuwepo tangu awali kuongeza ukubwa wa Mashamba yao ili kuhakikisha wanajipatia fedha nyingi ili kuongeza kipato chao na hatimaye kuongeza uwezo wa kupata mahitaji Muhimu pamoja na kujikimu Kimaisha
Timu ya wadau wa Tumbaku katika mkoa wa kitumbaku Chunya kila mwaka hufanya tathimini ya uzalishaji wa zao la tumbaku kwa wakulima na takwimu zinazopatikana kutokana na zoezi hili husaidia wadau wa Tumbaku kuweka vizuri mipango ya Masoko, pia zoezi hili linasaidia wakulima kupa ushauri kitaalamu pale panapobidi ili wawezekupata tija
Zoezi hili linatarajia kukamilika kwa muda wa siku Kumi na nane (18) ambapo vyama vyote Ishirini na moja vilivyopo katika halmashauri ya wilaya ya Chunya vitafikiwa na zoezi hili muhimu
Vijana wanaojishughulisha na kilimo cha Tumbaku wilayani Chunya wamekiri wazi kwamba kilimo kwao ni ajira na kinawalipa kuliko kuajiliwa na wamewataka vijana wenzao kuja Chunya kuwekeza kwenye kilimo kuliko kubaki mjini na huna ajira.
“Watu wengi wanaifahamu Chunya kwa upande mmoja tu wa uchimbaji wa dhahabu hivyo kusahau uwepo wa kilimo lakini mimi nikusisitizie kwamba Chunya kuna hazina kubwa sana katika kilimo, Upande wangu mimi kilimo kinanilipa sana na ndio sababu mwaka huu nimeamua kulima hrka ishirini za Tumbaku (20)”
Ni dhamira ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, kumletea maendelo mwananchi wake bila kujali eneo alipo (Mjini au Kijijini) na ili kufanikisha hilo kila mtu anapatiwa mahitaji muhimu kufanikisha shughuli anayoifanya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.