Halmashauri ya wilaya ya Chunya imetoa chanjo ya Surua Rubella kwa watoto 44,942 sawa na asilimia 116.37 wakati lengo lilikuwa kuwafikia watoto 38,619 na kwa takwimu hiyo Halmashauri ya wilaya ya Chunya imekuwa ni Halmashauri iliyochanja watoto wengi kuliko wilaya nyingine yoyote ya Mkoa wa Mbeya ukilinganisha na malengo yaliyokuwa yamewekwa awali
Akitoa taarifa ya zoezi la chanjo mratibu wa Huduma za Chanjo Halmashauri ya wilaya ya Chunya Blasio Kabwebwe amesema Halmashauri ya wilaya ya Chunya ni kati ya wilaya Ngumu kuwafikia wananchi katika maeneo yao kwani kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kuna umbali mrefu lakini juhudi, kujituma na hata moyo wa uzalendo wa maafisa wanaohusika na zoezi la Chanjo ndiyo msingi wa kufikia lengo na hata kuvuka kiwango kama takwimu zinazoeleza
“Kuwafikia wananchi wa Chunya kwa kiwango hicho sio kazi ndogo maana wilaya ya Chunya inajulikana wazi kwa jiografia yake lakini lazima nipongeze kazi kubwa iliyofanywa na wataalamu ambao wamehusika katika zoezi la Chanjo, wamejituma sana na kwa moyo wa uzalendo na matokeo yake ndo hayo katika mkoa tumefanya vizuri kuliko wilaya nyingine” Amsema Kabwebwe
Aidha Kabwebwe ameshukuru uongozi mzuri na bora kutoka kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya, Mkurugnezi mtendaji wa Halmashauri na viongozi wote ambao wameshiriki kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha zoezi la Chanjo linafanikiwa kwa kiwango kikubwa kiasi cha wilaya ya Chunya karibu mara kadhaa sasa huwa tunaongoza mkoa wa Mbeya
“Lazima nitambue uongozi mahiri wa Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya Dr Drison Andrew katika zoezi hili, nitambue pia usimamizi wa Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Chunya Ndugu Tamim kambona nna viongozi wengine wote kuanzia ngazi ya wilaya, kata, vijiji pamoja na wananchi kwa ujumla naweza kusema bila watu hao niliowataja na wengine ambao sijawataja ndio wamefanikisha zoezi hili kwa ukubwa huo” Aliongeza Kabwewe
Samweli Macha aliyekuwa kituo cha Mafyeko na Tumain Mbaba aliyekuwa kituo cha Mkola kwaniaba ya wataalamu wote waliohusika kwenye zoezi la Chanjo ya Surua Rubella wamesema zoezi limefanyika vizuri chini ya usimamizi mzuri wa viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya, viongozi wa kata na Vijiji, huku wakisema wananchi wametoa ushirikiano mzuri ambao umepelekea kuvuka lengo lililokusudiwa
Zoezi la Chanjo ya Surua Rubella zimeendeshwa nchi nzima ambapo lilianza rasmi tarehe 15/2/2024 na kuhitimishwa leo tarehe 18/2/2024 na walengwa walikuwa watoto wenye umri wa miezi tisa 9 mpaka miezi 59 ambapo vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo yaliyokubalika yalitumika kutoa chanjo huku wilaya ya Chunya Ikifanikiwa kufanya vizuri kwenye zoezi hilo kwa kuvuka lengo ambapo imewafikia watoto 44,942 kati ya watoto 38619 waliokusudiwa.
Tumain Mbaba (Afisa anayemchoma sindano mtoto) akiwa anaendelea kutekeleza jukumu lake leo tarehe 18/2/2024 katika kata ya Mkola wakati wa zaoezi la Chanjo ya Surua Rubella
Samwel Macha (Anaye mchoma mtoto Sindano) akiendelea kutekeleza jukumu la Chanjo ya Surua Rubella ikiwa ni siku ya mwisho leo tarehe 18/2/2024 katika kituo cha Mafyeko
Wanaume wilayani Chunya wamekuwa na mwamko katika kushiriki Chanjo mbalimbali ili kuhakikisha Familia wanazoziongoza zinakuwa salama, Picha hapo juu ni kati ya picha mbalimbali zinazoonesha namna ambavyo wanaume wamekuwa mstari wa mbele kupeleka watoto katika kupata chanjo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.