Halmashauri ya wilaya ya Chunya timu ya wanaume kuvuta kamba imetinga FAINALI baada ya kuwapiga nje ndani wapinzani wote waliokutana nao kwenye Mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea jiji Dododma ambapo moja ya vibonde wa Chunya ni timu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaama maarufu kama Dar city council nao wamepigwa nje ndani.
Safari bya Timu hiyo tangua hatua za awali imekutana na timu kutoka Halmashauri Mbalimbali na kuzichalaza bila Huruma kwa ushindi wa Mbili bila kwa kila timu waliyokutana nayo jambo linalofanya Chunya kuendelea kuwa na uhalali wa kuendelea kutetea Ubingwa huo kwa mashindano ya SHIMISEMITA mwaka 2023 ambayo yataraji kutamatika hivi punde.
Hebu fuatilia safari ya Chunya DC timu ya wanaume kuvuta Kamba mpaka kutinga Fainali.
Hatua ya Makundi Mshindi CHUNYA DC alivuka hatua hiyo kwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye kundi lake.
Hatua ya Kumi na sita Bora (Mtoano) Moshi Dc Vs Chunya Dc Mshindi CHUNYA DC
Hatua ya Robo Fainali DAR CC VS Chunya DC Mshindi CHUNYA DC
Hatua ya Nusu Fainali Chunya DC vs muleba Mshindi CHUNYA DC
Sasa Fainali ni kesho CHUNYA DC vs BARIADI DC Je ni Chunya DC BINGWA? Tukutane kesho Jumapili tarehe 29/10/2023
Haya ni maneno ya kepteni timu ya kuvuta kamba wanaume Ridhiwani Mshighati “Kabla ya mchezo wa leo tumekaa vikao kwaajili ya mikakati na tumekubaliana leo tunashinda na ni kweli tumeshinda, na tunahakikisha tupumzika vya kutosha huku yeyote anayetoka kambini ni kwa ruhusa maalumu na tukimaliza mchezo wa kesho ndipo watu waendelee na mambo mengine.
Mchezo Mgumu kuliko michezo yote ilikuwa ni kati yetu Chunya DC vs Dar CC, baada ya mchezo nimefuatilia takwimu kuna wakati raundi ya kwanza kamba ilisimama haiendi kwao wala kwetu kwa sekunde 48 jambo ambalo nafikiri halijawahi kutokea katika mashindano haya, tuliporejea raundi ya pili ndani ya sekunde kumi tu tulikuwa tumeshawashinda wapinzani wetu.
Lakini nashukuru sapoti kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kupitia kwa afisa michezo wa mkoa kwani mara Mara amekuwa akitupigia simu, amekuwa akiuliza matokezo mbalimbali na amekuwa akituhamasisha na kutupa mbinu mbalimbali katika michezo mbali maana yeye pia ni mzoefu katika mambo ya michezo na ametuahidi kama tukifanya vizuri tunataraji kupokelewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kwetu sisi hii tunaona ni hamasa kubwa” Alisema Mshighati.
Kwa niaba ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Afisa Michezo wa Mkoa wa Mbeya Bwana Robert Mfugale amesema jambo walilolifanya Halmashauri ya wilaya ya Chunya kupitia uongozi wake kwa ujumla ni jambo la kuigwa huku akisema wametimiza wajibu wao vizuri maana kitendo cha Kusafirisha timu ya watu 35 kwenda Dododma kushirki Michezo inapswa kuigwa na Halmashauri zote zinazounda Mkoa wa Mbeya.
“Mimi kwanza nisema kwa maana ya Mkoa wa Mbeya tunaipongeza Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa maana ya uongozi wote wa Halmashauri kwa kuona umuhimu wa mashindano haya hatimaye kuruhusu timu ya watu 35 kusafiri kwenda kushiriki mashindano haya na kwa taarifa nilizonazo kati ya timu zilizosafiri kitajiri ni hii ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwani wamelipwa stahiki zao zote, na wamesafiri kwa Basi lao toka Chunya na basi hilo wanalo Dodoma linaendelea kuwazungusha viwanja vya mazoezi na kuwarudisha kambini yaani niseme Chunya wameuheshimisha Mkoa wa Mbeya huko Dododma.
Sisi kama Mkoa tunawapongeza sana viongozi wa Chunya kwa Kutimiza wajibu wao lakini pia tunawapongeza watumishi waliokwenda kushindana wametimiza pia wajibu wao. Na kwa taarifa nilizo nazo tayari tuna washindi wa tatu kwa timu ya wanawake kuvuta kamba, mshindi wa tatu kurusha tufe na tayari timu ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeingia Fainali kuvuta kamba wanaume. Sisi kama mkoa tukiona inafaa na ratiba ikaruhusu pande zote mbili basi tutawaalika wanaporudi wapitie hapa ili viongozi wawapongeze ndipo waendelee na safari ya kurejea Chunya”. Alisema Robert Mfugale.
Mwana Chunya, Mwana Mbeya Timu ya Halmashauri ya Chunya hata kama sio moja kwa moja, inawakilisha Mkoa wa Mbeya kwenye Mashindano yanayoendelea Dodoma, Maandalizi yote yamekamilika lakini maombi yako wewe mwenye Mapenzi mema na Chunya na mwenye Mapenzi mema na Mkoa wa Mbeya iombee timu ya Chunya ichukue ubingwa tena.
Mpaka sasa Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeshinda Mshindi wa tatu wanawake kuvuta kamba, nafasi ya Tatu Kurusha Tufe, Mdhindi wa kwanza kurusha tufe ametoka Mbeya (Rungwe) na sasa Chunya tuko Nusu Fainali mchezo wa Draft na Mvhezo wa Vukuta Kamba wanaume tutacheza Fainali kesho tarehe 29/10/2023 saa kumi na Mbili asubuhi.
Timu ya wanaume kuvuta kamba ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya ikiwa katika katika maandalizi ya kuwabuluza wapinzani wao huko SHIMISEMITA DODOMA
Timu ya wanawake kuvuta kamba ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya chini ya kepteni wake Devotha Mwasaga (Wa pili kutoka kushoto) wakisiliza maelekezo katika moja ya michezo yao huko Dodoma
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.