Afisa utumishi na Rasimali watu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu John Maholeni amewataka wajumbe wa kikao cha ya Afya Msingi wilani Chunya kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wataalamu wa Afya katika mapambano ya Polio Jambo litrakalo leta ufanisi katika mapamano hayo
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 15/09/2023 alipomuwakilisha Mkurugenzi mtendaji katika kikao cha ya Afya Msingi kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya uliopo jingo jipya la utawala la wilaya ya hiyo na kuhusisha wajumbe mbalimbali wakiwepo watendaji wa kata, viongozi wa dini, wataalamu wa Afya na wadau wengine
Naye Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Dr Darison Andrew amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya kushirki kwa ukamilifu katika zoezi la Chanjo ya Polio inayotaraji kufanyika kuanzia tarehe 21-24 septemba 2023 ambapo vituo vyote 31 vya kutolea Chanjo vitahusika
“Tunalo jukumu kwa pamoja kuhakikisha watoto chini ya miaka 8 wanapatiwa Chanjo kwani nao wako katika hatari kubwa ya kupata Ugonjwa huo na Lengo letu ni kuhakikisha elimu kuhusu Ugonjwa wa polio na chanjo inawafikia wananchi kikamilifu kwani ugonjwa huu hauna tiba bali unaweza kuzuilika kwa kupitia Chanjo na athari zake kubwa kama vile kupooza, ulemavu wa kudumu na hata kufa”
Aidha Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya amewataka watendaji wa kata, viongozi wa dini pamoja na watoa huduma za afya kupambana na ugonjwa wa polio kwa Pamoja ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kwa jamii yetu lakini amewataka watoa huduma za afya kuhakikisha Chanjo zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Miongozo zinapatikana maeneo ya vituo vyao.
“Ni kazi yenu wataalamu wa Afya kuhakikisha chanjo zinazotakiwa kuwepo eneo la kituo chako zinakuwepo lakini pia kupitia kamati za afya ngazi za kata mpaka vijiji washirikishwe nao wasaidie kuhakikisha wananchi wanafika kupata huduma ya Chanjo”
Wajumbe wa kikao hicho wamejitokeza kuchangia ili kuboresha maeneo mbalimbali ili kuhakikisha zoezi linakuwa la mafanikio na linafikia lengo ambalo Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania linafikiwa na hatimaye wananchi wanakuwa salama kiafya na waendelee na uzalishaji mali
Kikao hicho kimehudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama, watendaji wa kata zote za wilaya ya Chunya, viongozi wa Dini zote yaani dini ya Kikristo na Dini Kiislamu, wahudumu wa Afya toka vituo vya kutolea huduma za afya na wajumbe mbalimbali wakiwepo Afisa usafirishaji, na wengine wengi
Mganga Mkuu wa wilaya ya Chuna Dr, Darison Andrew akifafanua jambo alipokuwa akifafanua umuhimu wa chanjo ya polia na namna ambavyo wilaya ya Chunya inatamani wajumbe wa kikao hicho wakashiriki katika mapambanoya polia wakati wa kikao
Winfrida Mwakabonga Muuguzi msaidizi Zahanati ya Mazimbo akichangia mada wakati wa kikao
Mratibu wa Huduma za Chanjo halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Blasio N. Kabwebwe akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa wakati wa kikao mapema leo
Wajumbe wa kikao cha Afya ya Msingi wakifuatilia kwa makini wakatiMganga Mkuu wa wilayta ya akitoa ufafanuzi wa umuhimu wa kushiriki na kushirikisha watu wengine Chanjo ya Polia inayotaraji kufanyika tarehe 21-24/09/2023
Wajumbe wa kamati ya afya ya msini wakigawiwa vipeperushi na mabango yanayohimiza wananchi kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki katika mapambanao ya Polia ambapo serikali inataraji kuratibu zoei la Chanjo kuanzia 21-24 september 2023
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.