Halmashauri ya Wilaya ya chunya imekamilisha mpango wake wa kununua magari mawili (2) mapya kwa kutumia mapato yake ya ndani kwa mwakwa wa fedha 2021/2022 lengo ikiwa ni kuboresha utoaji wa huduma pamoja na ukusanyaji wa mapato
Magari hayo ni Toyota Hilux double cabin pick up kwa gharama ya sh. 92,346,913.16, Totota Land Cruiser Hardtop kwa gharama ya Tsh. 168,542,585.44, ambapo magari yote mawili yamegharimu Tsh. 260,889,498.6.
Aidha mchakato wa manunuzi ya magari hayo ambayo ni moja ya nyenzo muhimu kwa halmashauti katika kutekeleza shughuli za kimaendeleo, umefanyika kwa kufuata taratibu zote za manunuzi ya umma, ikiwa nipamoja na kuomba kibali cha kufanya manunuzi kutoka katika Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde akifanya majaribio moja ya gari zilizo nunuliwa na halmashauri kwa kupitia mapato yake ya ndani.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.