Kituo cha afya Sangambi kilichojengwa kwa fedha za mapato ya Ndani kitafunguliwa rasmi tarehe 1/4/2023 ili kuendelea kumrahisishia mwananchi wa Sangambi kupata huduma ya Afya kama ilivyo azma ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.
Akitoa taarifa Mbele ya Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Chunya Afisa Elimu Kata ya Sangambi Mwalimu JOSEPH KIHWELE akimuwakilisha Afisa mtendeji kata hiyo ndugu Ntundu Chapa amesema kwasasa wako hatua za mwisho za kukamilisha matengenezo madogo madogo ambapo kufikia tarehe 1/4/2023 kituo kitaanza kufanya kazi
Mwalimu KIHWELE amesema wanaishukuru sana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuruhusu halmashauri kupitia makusanyo ya ndani kujenga vituo vya afya ambapo Kata ya Sangambi inakuwa ni kati ya kata za kwanza Tanzania kupata Faida hiyo lakini pia tunashukuru uongozi wa Halmashauri ya wilaya kutoa fedha hizo
“Tunashukuru serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoongozwa na Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi bora pamoja na utoaji wa fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendelo katika halmashauri yetu. Pia tunaishukuru Halmashauri ya wilaya kwa kutoa fedha za ujenzi wa kituo hiki cha Afya kata ya Sangambi kwa Mwaka wa fedha 2022/2023”
Wajumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Chunya iliyoongozwa na katibu wa chama hicho ndugu Charles Jokery kwanza wamepongeza serikali kuruhusu halmashauri kutumia fedha za mapato ya Ndani kujenga vituo vya afya na pia wamepongeza ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu Kambona aliyewakilishwa na Afisa Mipango Godfey Africa Mwakibinga kwa usimamizi mzuri wa mradi huo
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi akijumuisha maoni ya wajumbe wa kamati ya siasa amesema mradi huo umetekelezwa kwa viwango vikubwa na unastahili pongezi nyingi kwani katika kila eneo walilokagua wameridhishwa sana
“Kama kamati ya siasa tumepitia vituo vya afya karibu vinne na miradi mingine mingi lakini hakuna mradi uliofanywa vizuri kama mradi huu wa kituo cha Afya Sangambi, Hivyo nikupongeze mkurugenzi na timu yako kwa ujumla kwa kazi hii nzuri na njema”
Aidha katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Chunya alimtaka Mkurugenzi kuhakikisha kituo kinaanza kutoa huduma kama ilivyokusudiwa ili kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa huduma za afya ambapo kwasasa wananchi zaidi ya elfu kumi (10,000) wanaitgemea zahanati moja wakati huduma nyingine kubwa mpaka kituo cha Afya Chalangwa au Hospitali ya wilaya Chunya ambapo ni umbali wa zaidi ya Kilomita thelasini (30) kufikia vituo hivyo
Mradi huo unakadiliwa kugharimu fedha shilingi milioni mia sita (600,000,000/=) kati ya fedha hiyo milioni mia tano (500,000,000=) ni fedha za mapato ya ndani kutoka halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati shilingi milioni mia moja (100,000,000/=) ni nguvu za wananchi.
Mpaka sasa mradi umegharimu shilingi milioni mia nne sabini (470,000,000/=) ambapo shilingi milioni mia nne ishirini na tatu (423,000,000/=) ni fedha kutoa mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati Nguvu za wananchi zikigharimu milioni arobaini na saba (47,000,000)
Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Chunya iko katika ziara ya kawaida ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa lengo la kujiridhisha kama miradi hiyo inathamani sawa na fedha ambazo serikali imeleta kujenga mirdi hiyo.
Muonekano wa Majengo katika kituo cha Afya Sangambi
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya wakiongozwa na Katibu wa CCM wilaya ya Chunya Ndugu Charles Jokery wa pili kutoka kushoto wakisikiliza taarifa ya ujenzi wa kituo cha Afya Sangambi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.